Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akiongea na Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo (hawapo pichani) pamoja na
wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika
Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Mwenyekiti
wa Bodi Hospitali ya Mirembe, Prof. Gadi Kilonzo akiongea na Wajumbe wa
Bodi ya Hospitali hiyo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa
kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe
Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Mganga
Mkuu na Katibu wa Bodi ya Hospitali ya Miremb, Erasmus Mndeme akiongea
na Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo (hawapo pichani) pamoja na wageni
waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya
Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Mkurugenzi
Msaidizi Hospitali ya Mirembe, Bibi. Doroth Gwajima akiongea na Wajumbe
wa Bodi leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya
Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma
08/02/2017.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy
Mwalimuakiwakabidhi vitendea kazi baadhi ya Wajumbe wa Bodi aliyoizindua
leo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya
Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi leo 08/02/2017 mkoani Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe
kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe
Mkoani Dodoma 08/02/2017. (PICHA/HABARI NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)
SERIKALI
imesema kwamba tatizo la maradhi yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya
akili yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku huku vyanzo vyake vikiwa ni
pamoja na urithi, matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, matatizo ya
kisaikolojia pamoja na hali ngumu ya maisha.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akizindua
Bodi ya Hospitali ya Mrembe Mkoani hapo.
Akiongea
na mbele ya Watendaji wa Bodi hiyo, wageni waalikwa pamoja na Viongozi
wa hospitalini hapo, Waziri Ummy amesema kuwa, kundi lililoathirika
Zaidi na kdhai hiyo ni vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa, ambapo
alitaja taarifa ya Shirikala Afya Ulimwenguni (WHO) ya mwaka 2016n
inayoonyesha takribani watu milioni 15.3 Duniani wanapata matatizo ya
kiafya yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya
pombe kupita kiasi.
“Matatizo
haya yamekuwa yakisababisha vifo milioni 3.3 kila mwaka Duniani kote,
hata hivyo taarifa ya Wizata yangu inaonyesha kwamba idadi ya watu
wanaougua magonjwa ya akili inaongezeka kwa kasi kubwa kutoka wagonjwa
136,710 mwaka 2011/2012 hado wagonjwa 448,997 mwaka 2015/2016”, alisema
Ummy.
Ameongeza
kuwa, takwimu za hospitali ya Mirembe zinaonyesha kuwa, katika kipindi
cha miaka mine kuanzia mwaka 2012 hadi 2016, jumla ya wagonjwa Zaidi ya
60,000 wenye magonjwa ya akili na waathirika wa dawa za kulevya
walipatiwa huduma za afya na utengamao.
Aidha,
kwa kutambua majukumu makubwa ya hospitali hiyo na kutatua changamoto
zinazohusiana na magonjwa hayo, Serikali imeamua kuunda Bodi ya
hospitalini hapo lengo likiwa ni kutekeleza dhana ya Utawala Bora na
Utoaji wa Huduma Bora za Afya ya Akili kwa mujibu wa mapango mkakati na
sera za nchi.
“Ninayo
furaja leo kushiriki nanyi katika uzinduzi wa Bodi hii ya Hospitali ya
Afya ya Akili Mirembe, na bodi hii itaongozwa na Mwenyekiti pamoja na
Wajumbe waliouteuliwa kutoka maeneo mbaimbali ya kiujuzi hapa nchini”,
alisema Waziri Ummy.
Amesema
kuwa, bodi hiyo itakuwa na majukumu mbalimbali yakiwemo kusimamia
utendaji wa hospitali hiyo na Taasisi ya Isanga, kuhakikisha kuwa Sheria
ya uanzishwaji wa hospitali inapatikana kwa wakati, kushauri kuhusu
muundo wa hospitali, kuunda kamati ndogo ndogo, kushauri kuhusu mpango
wa muda mrefu ili kuboresha huduma pamoja na kushauri jinsi ya kupunguza
gharama za uendeshaji hospitalini hapo.
Sambamba
na kuzindua bodi hiyo, Waziri Ummy ameitaka jamii kushirikiana na
Serikali katika kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya hususan kwa
vijana ili nguvu kazi ya Taifa isizidi kupotea.Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Gadi Kilonzo amempongeza Waziri Ummy na
kwa kuzindua bodi hiyo na amemuhakikishia kuwa bodi hiyo itatekeleza
maagizo yote pamoja na majukumu iliyopewa ili kuboresha utendaji kazi
hospitakini hapo.
“Dhama
uliyotupa sisi Wajumbe wa Bodi ni kubwa, tunaieheshimu sana na pia
nakuahidi kuwa, tutatekeleza kwa bidii majukumu yote ya kuisimamia
hospitali hii, tutajitahidi kwa uwezo wetu wote kutatua changamoto za
hospitali hii kwa kushirikiana na wadau wengine wa afya kupitia Wizara
yako, pia tunashukuru kwa vifaa vya kazi ulivyotupatia kwa ajili ya
kutumia wakati wa utendaji wetu”, alisem Kilonzo.
Wajumbe
waliochaguliwa kuunda bodi hiyo ni Profesa Gadi Kilonzo ambaye ndio
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt. Erasmus Mndeme ambaye ni Katibu wa Bodi na
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mirembe, Dkt. Mpona Boniventura ambaye ni
Mwakilishi kutoka chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Joseph Mbatia, Ndugu
John Sipendi, Ndugu Ernest Kabohola, Ndugu Jane Magembe pamoja na Ndugu
Clavery Lyela.
No comments:
Post a Comment