MKE
wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wametoa wito kwa Watanzania kujengea utamaduni wa kutembelea
vituo vya wazee na watu wenye mahitaji maalumu na kutoa misaada ili
waweze kujikimu.
Wameyasema
hayo leo (Jumatano, Februari 15, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya
Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Amani
Ipuli yaliyoko kwenye Manispaa ya Tabora mkoni Tabora.
Katika
makazi hayo wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele,
unga wa sembe na maharage pamoja na mafuta maalumu kwa ajili ya watoto
wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule mbalimbali mkoni Tabora.
Hata
hivyo, Mama Janeth amewapongeza watumishi wote wanaofanyakazi kwenye
makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu kwa sababu kazi
hiyo ni ngumu na ina changamoto nyingi.“Ibada
si kwenda katika nyumba za ibada pekee bali hata kuwatembelea wazee,
watu wenye mahitaji maalumu na wasiojiweza utakuwa umetoa sadaka kubwa
kwa Mwenyezi Mungu. Nawaomba tujitahidi kuwatembelea,” amesema.
Kwa
upande wake Mama Mary amewaomba wananchi wote wawe na utaratibu wa
kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulele wazee, walemavu na
wasiojiweza nchini na kuwafariji kwa sababu wanahitaji upendo na faraja
kutoka kwao.
Pia
Mama Mary ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto pamoja na wadau mbalimbali kwa kujitoa kwa hali mali katika
kuwahudumia wazee na watu wenye mahitaji maalumu.Naye
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt.
Hamis Kigwangala amesema Serikali itahakikisha huduma zinaboreshwa
katika makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu nchini kwa
kuwa vingi viko katika hali mbaya.
Awali
Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Tabora, Bw. Baraka Makona alisema makazi
hayo yalianzishwa mwaka 1969 kwa lengo la kuwasaidia watu wasiojiweza
hususan walioathirika na ugonjwa wa ukoma ambao walitengwa na familia
zao.
Bw.
Makona alisema baada ya ugonjwa wa ukoma kupungua mkoani Tabora kwa sasa
makao hayo yanahudumia wazee wasiojiweza wenye ulemavu na ambao
wametengwa na jamii kutokana na sababu mbalimbali.
Katika
hatua nyingine, Bw. Makona alisema makazi hayo yanakabiliwa na
changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa majengo, ukosefu wa gari
la wagonjwa hali inayosababisha usumbufu mkubwa hasa inapotokea dharura
nyakazi za usiku kwani hakuna zahanati karibu na makazi hayo.
Pia
Bw. Makona amewapongeza wake wa viongozi hao kwa moyo wao wa dhati wa
kuamua kutembelea makazi hayo na kutoa misaada mbalimbali vikiwemo
vyakula kwa sababu wameonyesha matendo ya huruma na Mwenyezi Mungu
atawabariki.
Naye
Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee George Busambilo
aliwashikuru wake hao wa viongozi kwa niaba ya wenzake na kuwaomba
waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji
maalumu.
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha
wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli
katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017

wakilakiwa kwa nderemo walipowasili katika kituo cha wazee na watu
walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa
ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
:Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Mhe. Aggrey Mwanri na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Queen Mlozi wakati
yeye na Mama Mary Majaliwa walipotembelea katika kituo cha wazee na watu
walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa
ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakilakiwa kwa nderemo walipowasili katika kituo cha wazee na watu
walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa
ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi na wazee wasiojiweza
wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na
ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora
leo Februari 15, 2017
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi pamoja na wazee
wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu
watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora
mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi pamoja na wazee
wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu
watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora
mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
Pamoja na naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hamisi
Kigwangwalla wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa tabora Mhe. Aggrey Mwanri
akianzisha harambe kwa ajili ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika
kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani
Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakiwakabidhi mafuta maalumu wawakilishi wa wanafunzi wenye ulemavu wa
ngozi walioalikwa kwenye hafla iliyofanyika katika kituo cha wazee na
watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika
Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakikabidhi sehemu ya msaada wao wa tani 7.5 ya vyakula katika kituo cha
wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli
katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakikabidhi sehemu ya msaada wao wa tani 7.5 ya vyakula katika kituo cha
wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli
katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
wakikabidhi sehemu ya msaada wao wa tani 7.5 ya vyakula katika kituo cha
wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli
katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
No comments:
Post a Comment