Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WAZIRI
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema wanatarajia
kufanya mapitio ya sheria zinazohusu sekta ya sanaa na burudani nchini
ili kutoa fursa kwa taasisi binafsi kuwekeza zaidi.
Katika
kufanya mapitio hayo wataangalia jinsi ya kufanyia kazi sheria mbovu
zinazokandamiza sekta ya sanaa na burudani nchini na kuziondoa kabisa
ili kuleta manufaa kwa wasanii na wadau wanaohusika na sanaa.
Nape
ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua rasmi
urushwaji wa matangazo ya Kombe la mataifa Afrika (AFCON) pamoja na
kumkabidhi bendera kwa msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum)
anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano hayo
yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon.
Amesema
wasanii na watu wengine kwenye sanaa wamekuwa wakifanya kazi kwa juhudi
kubwa licha ya kutofaidika na kazi wanazozifanya na hatimaye wakijikuta
wakiwa chini kadri siku zinavyozidi kwenda mbele.
Amesema
serikali imedhamiria kushughulikia masuala yote yanayofanya wasanii na
wadau wngine kuwa wanyonge kutokana na uwepo wa sheria hizo.
‘Natambua
Kampuni ya Multichoice kupitia king’amuzi chake cha DStv katika
kuhakikisha wanakuza na kuendeleza masuala ya michezo na burudani
nchini, na sisi kuonesha tunaunga mkono jitihada zao tutapitia sheria
zote ambazo zimekuwa ni kikwazo kwenye ukuzaji tasnia ya sanaa hapa
nchini’ amesema Nape.
Nape
alimpongeza Diamond Platnum kwa kupata nafasi ya kwenda kutumbuiza
katika mashindano hayo na kudai kuwa kitendo hicho kinaipa faraja
Tanzania licha ya kuwa hawajapeleka timu katika mashindano hayo makubwa
barani Afrika.
Nae
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Salum Salum
amesema watanzania wataweza kujioneamashindano hayo Mubashara kutoka
nchini Gabon kupitia king’amuzi chao cha DStv kwenye kifurushi cha bei
ya chini cha Shilingi 19,975 pekee.
Amesema
kampuni hiyo itagharamia tiketi za watu sita kutoka kundi la WCB ili
kufanikisha adhma ya msanii Diamond Platnum kufanya shoo yenye uwezo wa
kuijulisha dunia kuwa Tanzania inavipaji vingi vya uimbaji mziki licha
ya kutopewa sifa katika baadhi ya maeneo mengine.
Aidha
Salum amesema mashindano yatakuwa yakionyeshwa mubashara(Live) ili
kuweza kutoa fursa ya watanania na kujikita zaidi kwenye michezo ili na
wao wapate nafasi ya kushiriki mashindano hayo katika kipindi cha miaka
ijayo.
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akizungumza wakati
wa hafla ya kumkabidhi bendera kwa msanii wa Bongofleva Nasib
Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa
mashindano hayo yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, akimkabidhi
bendera msanii wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda
kutumbuiza katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14
nchini Gabon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Salum Salum akizungumza
wakati hafla ya kumkabidhi bendera msanii wa Bongofleva Nasib
Abdul(Diamond Platnum)anayekwenda kutumbuiza katika ufunguzi wa
mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Msanii
wa Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza
katika ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon
akizungumza na waandishi habari juu ya safari hiyo leo jijini Dar es
Salaam.
Balozi
DSTV, Joti akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera msanii wa
Bongofleva Nasib Abdul(Diamond Platnum) anayekwenda kutumbuiza katika
ufunguzi wa mashindano yatakayofanyika Januari 14 nchini Gabon
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment