Mbunge
wa jimbo la Chalinze, Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Mwanasheria
Ridhiwani Kikwete akizungumza na baadhi ya wakaazi wa kijiji cha Ruvu
Darajani alipokwenda kwa ajili kusikiliza mkutano wa kusomwa mwa mapato
na matumizi ya kijiji ikiwa ni utekelezji wa agizo lililotolewa na Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj Hemed Majid la kuwataka viongozi wote wa
vijiji vinavyounda wilaya hiyo kuitumia siku ya Jan 3 kuwasomea mapato
na matumizi wannchi wao, hata hivyo mkutano huo umesogezwa mpaka
Alhamisi ya Jan 5.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze, Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Mwanasheria
Ridhiwani Kikwete akiwaunga mkono wafanyabiashara wa samaki wa kukaanga
wanaofanya biashara zao katika eneo la Ruvu Darajani pembezoni kidogo
mwa barabara Kuu ya Dar es Salaam- Chalinze, Morogoro- Segera,
alipowatembelea kushuhudia wanavyofanya shughuli zao hizo.
Mbunge
Ridhiwani Kikwete akiwasikiliza wafanyabiashara waaouza bidhaa
mbalimbali hapa wauza bidhaa jamiyambogamboga wakizungumza na mbunge
wao.
Na Omary Mngindo, Ruvu
MBUNGE
wa Jimbo la Chalinze Mkoa wa Pwani Mwanasheria Ridhiwani Kikwete Jan 3
amewatembelea wafanyabiashara katika kijiji cha Ruvu Darajani, Kata ya
Vigwaza Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani huku akiwaomba wawe
wanahudhulia mikutano inayoitishwa na viongozi wao.
Ridhiwani
amefika kwenye kijiji hicho kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa
agizo lililotolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj Hemed Mwanga
linalowataka wenyeviti wa vijiji na vitongoji wilayani humo kuitumia
siku ya Jan 3 kuwa maalumu kwa ajili ya kuwasomea wananchi wao mapato na
matumizi ili wananchi wao watambue makusanyo na matumizi yake.
Hata
hivyo Ridhiwani alipofika mweAnye Makao ya ofisi ya kijiji hicho
kinachongoza na Kambona Kwalo na ofisa Mtendaji wake Williamu Jeuli,
mkutano haukufanyika kwa madai ya wananchi hao kugoma kusomewa wakidai
kwanza lizungumzwe suala la mgongano unaohusha ardhi kati ya wananchi
haona mmoja wa wakazi anateishi jijini Dar es Salaam wakidai ni la muda
mrefu huku kukiwa hakuna utekelezaji wake.
Baada
ya kushindikana kufanyika kwa mkutano huo, Mwanasheria huyo aliamua
kufanya ziara ya papohapo ya kuwatembelea wafanyabiashara wanaofanya
shughuli zao katupika soko la Ruvu Darajani ambapo pia alitumia fursa
hiyo kuwaomba vijana kuwa na utamaduni wa kuhudhulia mikutano ya
setikali ya kijiji kwani ndipo sehemu ya kuibua miradi kwenye eneo lao.
Akizungumza
na vijana hao Ridhiwani alisema kwamba kwa utaratibu ambao vijana na
baaddhi ya wakazi hao ya kutohudhulia mikutano kwenye eneo lao
kutawafanya kukikosesha maendeleo kwa sababu kila jambo la maendeleo
linaibuliwa kwenye mikutano hivyo ni vema wakaweka itikadi zao pembeni
katika masuala yanayohusu maendeleo.
"Vijana
wenzangu katika suala linalohusu maendeleo tuweke pembeni itikadi zetu
binafsi, kwani katika maeneo yeyote ambayo mnayaona au kuyasikia yana
mafanikio makubwa, chanzo kikuu ni watu wake kuitikia wito wa kuhudhuria
mikutano kwani hapo ndipo wanapokaa na kukubalia jambo gani lifanyike
au la, kwa utaratibu ambao mnauendeleza wa kutohudhulia mikutano
mtaendelea kukidhohofisha kijiji chetu," alisema Mwanasheria huyo.
Alimalizia
kwa kuwaomba wajitokeze kwa wingi siku ya Alhamisi katika mkutano
utaofanyika kwenye ofisi ya kijiji chao ili waweze kuibua miradi
yakimaendeleo badala ya kukaa vijiweni na kuendeleza migomo ya kutofika
kwenye mikutano kwani hatua hiyo isiyo na yija itaendelea kukikosesha
maendeleo kijiji chao.
No comments:
Post a Comment