Rais mpya
wa Ghana ambaye aliwahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu hapo zamani,
Nana Akufo-Addo, ameapishwa rasmi leo kuwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo,
katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Independence Square Jijini
Accra, Ghana na kuhudhuriwa na viongozi kadha wa Afrika.Katika hotuba
yake ya kwanza, Nana Akufo-Addo, alimsifu rais aliyemaliza muda wake
madarakani, John Dramani Mahama, kwa namna alivyokiri kushindwa katika
uchaguzi wa mwezi uliopita.Viongozi zaidi ya 14 kutoka nchi za Afrika
walikusanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za
kuapishwa kwa rais huyo mpya, Nana Akufo Addo.
Rais Akufo Addo, alimshinda Rais John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Baada ya
kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili
namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka
madarakani.
Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.
No comments:
Post a Comment