Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza kwenye kikao cha kutatua migogoro ya Ardhi mkoani humo. |
Serikali
mkoani Arusha imejipanga ndani ya kipindi cha miaka miwili iwe imekomesha
migogoro ya ardhi sanjari na mivutano ya mikapa ya kiutawala kati ya
wilaya moja na nyingine.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo alisema hayo kwenye kikao cha
Ardhi,Kilimo,Mifugo na Mazingira kilichowaleta pamoja wakuu wa
wilaya,Wakurugenzi na Wenyeviti wa halmashauri pamoja na maafisa wengine
kujadili kwa kina mbinu za kumaliza migogoro hiyo.
Alisema
baada ya uhakiki wa mipaka na ushauri kutolewa eneo husika lipo Kijiji
au wilaya fulani kiongozi au mwananchi atakayehamasisha uvunjifu wa
amani atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Awali
Mpima Ardhi mkoa wa Arusha,Hamdoun Mansoor akiwasilisha taarifa ya
sekta ya ardhi alisema imekua ikitoa maelekezo ya kusimamia uendelezaji
katika maeneo ya vijiji na miji kwa kuzingatia sheri ya ardhi namba 5 ya
ardhi ya vijiji na 4 ya mwaka 1999 kanuni na taratibu zake.
Alisema
changamoto inayoikabili sekta yake ni ujenzi holela unaofanyika kwa
kasi kubwa katika maeneo ambayo kisheria yametangazwa kuwa maeneo ya
Mpango,ambayo hayaruhusiwi kuendelezwa bila kupata kibali kutoka kwenye
mamlaka husika.
"Serikali
hujikuta ikilipa fidia zisizo za lazima wakati wa kuendeleza
miundombinu mbalimbali na inapotaka kupeleka huduma nyingine za kijamii
kwenye maeneo hayo,"alisema Manssor
Aliyataja
maeneo ya umma yanayopaswa kuhifadhiwa kuwa ni pamoja hifadhi za
misitu,maeneo oevu,maeneo yenye vilima,vyanzo vya maji,mabonde na kingo
za mito.
Manssor
alisema uwezo mdogo wa halmashauri kulipa fidia umefanya maendeo mengi
kutopangwa na kupimwa na hivyo kuruhusu ukuaji wa kasi wa makazi holela
katika maeneo mengi ya mkoa na wilaya zake.
Migogoro
ya mipaka ngazi ya mkoa ni katika vijiji vya
Ngabobo,Olkung'wado,Leguruki,Ngejusosia,Miririnyi wilayani Arumeru
mkoa wa Arusha na Kijiji cha Lekirimuni wilaya ya Siha mkoa wa
Kilimanjaro ambayo inasababishwa na tofauti ya matangazo ya serikali
namba 135 la mwaka 1954.
No comments:
Post a Comment