Mbwa
ni mnyama kama wanyama wengine ambao huweza kupata magonjwa mbalimbali
ambayo hupelekea kufa au kuwapa vilema vya maisha. Mbwa ni kama binadamu
yoyote tu ambaye akishambuliwa na magonjwa basi anaweza kuwa dhaifu na
kupelekea kupoteza maisha au kupona lakini pia ni wanyama kama binadamu
tu wengine ambao hata wakipatwa na baadhi ya magonjwa basi wanaweza
kustahimili na kupona kabisa.
Basi
leo tutaangalia baadhi ya magonjwa yanayowapata viumbe hivi
vinavyopendwa sana na rafiki mkubwa wa binadamu. Kama ilivyo kwa wanyama
wengine na binadamu ugonjwa uanza kuonekana kutokana na dalili flani
ambapo ndio zinakupa taarifa za kuhisi kuwa mnyama huyu ni mgonjwa.
Lakini kuna baadhi ya magonjwa ukiona dalili zake basi unajua kabisa
kuwa ishatafuna sehemu kubwa na kupona ni majaaliwa na hali ipo hivyo
hivyo kwa wanyama kama Mbwa.
Tuanze na Huu leo
1:Parvovirus Infection (Kwa kifupi uitwa Parvo)
Ugonjwa
huu ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambapo mara nyingi hushambulia
mbwa wadogo wenye umri wa kuanzia wiki sita mpaka miezi sita. Ugonjwa
huu ni moja ya ugonjwa mbaya sana kwa mbwa kwasababu unapomuingia tu
basi matumaini ya kupona kwa mbwa huyo ni madogo sana kwasababu ni
ugonjwa ambao ukimpata mbwa ndani ya masaa 24 unaweza kupelekea kifo kwa
mbwa huyo.
Ugonjwa
huu husambulia sana mapigo ya moyo na kupelekea mapigo ya moyo ya mbwa
huyo kwenda mbio sana, na kumfanya hapoteze hamu ya kula, joto kushuka
sana.
Hizi
ndio dalili kubwa sana za ugonjwa huu wa Parvo ni Kuharisha damu,
Kutapika, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito ghafla. Mara umuonapo mbwa
wako ana dalili hizi basi unashauriwa kuwasiliana na mtaalamu wako wa
wanyama kwaajili ya ushauri na matibabu zaidi ijapokuwa kama mbwa huyo
hakuwahi kupatiwa chanjo ya Ugonjwa huo tokea utotoni basi asilimia ya
kupona ni ndogo sana kwa maana unapoona dalili za ugonjwa huu basi ni
dhahiri unakuwa ushamshambulia sana mbwa huyo.
Nini husababisha ugonjwa huu wa Parvo?
Mara
nyingi ugonjwa huu usababishwa na mbwa aliyehathirika moja kwa moja na
ugonjwa huu japokuwa kuna sababu nyingine kama endapo mbwa aliyeathirika
na ugonjwa huu anapojisaidia haja kubwa na mbwa mwingine akapita kunusa
basi mbwa huyo anakuwa anaambukizwa moja kwa moja. Inasemekana virus
vya ugonjwa huu vinauwezo wa kuishi kwenye udongo kwa takribani mwaka
mmoja na ugonjwa huu unaweza kuambukizwa moja kwa moja kutoka kwa mbwa
mmoja kwenda kwa mbwa mwingine.
Vilevile
Ugonjwa huu unaweza kuletwa na viatu endapo mtu amekanyanga kinyesi cha
mbwa aliyeathirika na ugonjwa huu basi anapoingia nyumbani au kwenye
mazingira ya mbwa ni rahisi sana kuacha virusi hivyo na ikumbukwe kuwa
virusi hivi huishi kwa takribani mwaka mzima kwenye udongo.
Unapohisi
umekanyaga kinyesi au kitu chochote ambacho kinaweza kuwa na virusi vya
parvo basi unashauriwa kusafisha eneo hilo kwa kutumia madawa ya kuua
virusi kwaajili ya kujirinda na ugonjwa huo hatari.
Vilevile
Kutompa chanjo sahihi mbwa wako na kwa wakati kunaweza kupelekea
kusababisha mbwa wako kupata ugonjwa huo, Kama unavyofahamu kuwa mbwa
wanatabia ya kunusa kila sehemu endapo bahati mbaya kanusa sehemu ambayo
tayari kuna virusi vya ugonjwa huo na hana chanjo basi ni rahisi
kushambuliwa na virusi hivyo.
Tiba ni Ipi kwa Ugonjwa Huu?
Inavyosemekana
mpaka sasa hakuna tiba sahihi ya ugonjwa huu lakini Mbwa anapozaliwa tu
na kufikisha muda wa wiki moja hadi mwezi unashauriwa kumpatia chanjo
mbalimbali kwaajili ya kumkinga na magonjwa kama haya na chanjo hio sio
ya mara moja tu anapochomwa mwanzoni basi unatakiwa kufata ushauri wa
mtaalamu wa wanyama kwa ratiba tena ya kurudia kumchoma chanjo katika
kipindi kijacho.
Aina hizi za mbwa ndio aina rahisi sana kushambuliwa sana na ugonjwa huu Rottweilers, Doberman Pinschers, Pit Bulls, Labrador Retrievers, German Shepherds.
Tukutane tena siku ijayo.
Je umeipenda makala hii?Basi unaweza kushare na Wenzako
Tu follow instagram kwa jina la @lukazablog @lukazablog @lukazablog
No comments:
Post a Comment