Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii
Waziri
wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amesema
amejifunza mengi kupitia kazi za mwandishi na mpiga picha wa kampuni ya
TheGurdianLtd marehemu Mpoki Bukuku kutokana na mchango wake mkubwa
katika tasnia ya habari.
"Bukuku
ameacha pengo kubwa hivyo hatosahaulika... wanahabari hatuna cha
kufanya ila tunamshukuru Mungu na kupitia kazi zake tujifunze yale yote
aliyoyafanya," alisema.
Akisoma
historia ya Bukuku, kaka wa marehemu, Alfred Mwakaposa alisema marehemu
alizaliwa 15/3/1972 katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha,
akiwa mtoto wa tano kwenye familia ya Bukuku.
Alisema
alianza elimu ya msingi katika Shule ya Forodhani, Mlimwa Dodoma na
baadae kuhamia Kisarawe, elimu ya sekondari alisoma Canon Andrea mkoani
Dodoma na kidato cha tano na sita katika Shule ya Makumira Arusha.
"Baadaye
marehemu alijiunga na elimu ya chuo cha uandishi wa habari TSJ ngazi ya
cheti na Diploma... Amewahi kufanya kazi katika gazeti la Majira,
Mwananchi na kuhamia Guardian mpaka mauti yalipomfika," alisema.
Akizungumza
kwa niaba ya wasanii wa filamu, Muigizaji maarufu Steve Nyerere alisema
tasnia ya filamu imepata pigo kubwa kumpoteza Bukuku hivyo wanaamini
anapoenda ni sehemu nzuri.
"Nimemjua Mpoki wakati tupo Singida, tunaamini anapoenda Mpoki ni sehemu nzuri, tuko pamoja na familia yake, " alisema.
Jeneza
lenye mwili wa mpiga picha maarufu Marehemu Mpoki Bukuku likiwa katika
eneo la uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu
tayari kwa kutoa heshima za mwisho
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye
akizungumza jambo wakati wa kuagwa kwa mwili wa mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku katika eneo la uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
akizungumza jambo wakati wa kuagwa kwa mwili wa mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku.
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mpoki Bukuku wakati wa kuagwa kwa mwili huo.
Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Lelo pamoja na Muwakilishi
wa Bloggers, Richard Mwaikenda akitoa salamu za rambirambi katika Msiba
wa Mpoki Bukuku, viwanja vya Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar.
Baadhi
ya waombolezaji wa wakiwa kwenye shughuli ya kuagwa kwa mwili wa
marehemu Mpoki Bukuku katika uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga
jijini Dar mchana huu.
No comments:
Post a Comment