Mradi
wa Wanawake Kwenye Usukani "WOMAN ON WHEEL" (WOW) umelenga kuwapa fursa
wanawake kujiajiri na kuajiriwa katika sekta ya usafirishaji kwa
kuendesha vyombo vya moto vya abiria na mizigo.
Mradi
wa WOW kwa sasa unasajili wanawake kwa ajili ya kuwapatia fursa ya
kufundishwa udereva bure katika viwango mbalimbali na baadae kuwatafutia
ajira na wengine kuwawezesha ili waweze kujiajiri.
Mradi
wa WOW umelenga katika kipindi cha mwezi Disemba hadi Februari uwe
umesajili wanawake 600 nchi nzima ili waweze kupatiwa mafunzo.
Lengo kubwa la mradi ni kuondoa mila potofu za mfumo dume wa uwepo wa kazi za kiume na kike.
Mradi
wa WOW utawezesha wanawake kushiriki kikamilifu kuchangia pato la taifa
kwa kujiwezesha kulipa kodi mbalmbali za serikali kupitia sekta ya
usafirishaji.
Martin
Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW)
akizungumza na washiriki wa semina hiyo ya siku moja hawapo pichani,
iliyolenga kuwapa fursa wanawake kujiajiri na kuajiriwa katika sekta ya
usafirishaji kwa kuendesha vyombo vya moto vya abiria na mizigo kupitia
mradi huo.
Martin
Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW)
akizungumza na washiriki wa semina hiyo ya siku moja , iliyolenga
kuwapa fursa wanawake kujiajiri na kuajiriwa katika sekta ya
usafirishaji kwa kuendesha vyombo vya moto vya abiria na mizigo kupitia
mradi huo.
Baadhi
ya wanawake washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifurahia maelezo
na umuhimu wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW).
Baadhi
ya wanawake washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifuuatilia
maelezo ya umuhimu wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW).
Victor
Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW)
akielezea jambo wakati alipotoa mafunzo kwa wanawake washiriki wa semina
hiyo.
Victor
Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW)
akifafanua jambo huku akisikilizwa kwa makini na baadhi ya washiriki.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia maelezo kutoka kwa Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW)
Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akitoa maelekezo kwa baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Victor
Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW)
akigawa baadhi ya vipeperushi vyenye maelezo muhimu kuhusu mradi huo.
No comments:
Post a Comment