| Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akifungua kikao cha kwanza cha Kamati ya Amani ya viongozi wa dini ofisini kwake. |
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo(kushoto) katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati (KKKT) mkoa wa Arusha. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo(katikati) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini
waliohudhuria Kikao cha Kamati ya Amani.
|
Nteghenjwa Hosseah –
Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Mashaka Gambo amekutana na kamati ya Amani ya Mkoa
ambayo inajumuisha viongozi wa dini mbalimbali zilizoko katoka Mkoa huu kuzungumzia
mustakabali wa Amani na namna viongozi hawa wa dini
watashirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo kwa
wananchi ambao ni waumini wao.
Akizungumza katika Kikao hicho Mhe. Gambo alisema kazi ya Ulinzi wa Amani itakua rahisi sana
kupitia viongozi wa dini ambao wana karama ya kuongea na kubadilisha
maisha ya watu bila kutumia nguvu ama kuwashurutisha isipokua kwa chakula
cha roho ambacho hujenga misingi imara ya imani na tabia njema.
Maendeleo ya wananchi hayawezi kupatikana bila Amani kuwepo
katika Mkoa wetu ni lazima tusaidiane katika hili dhamira yetu ifanikiwe kwa
wepesi zaidi tuna Imani kubwa sana Na viongozi wetu wa dini na ndio maana
nikaona ni vyema tukakutana ili tusikie kutoka kwenu ninyi ambao mnawakilisha
kundi kubwa la wananchi na pia kufahamu kero mbalimbali zinazowakwaza wananchi
katika maeneo yenu alisema Gambo.
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati KKKT Solomon Masangwa
akichangia kuhusu masuala yanayoweza kuhatarisha amani alisema kundi
ambalo linatakiwa kuangaliwa kwa jicho la Tatu na litasaidia sana katika
ulinzi wa Amani ni waendesha boda boda pamoja na wanachinga ambao kwa sasa
wanaonekana kutopewa kipaumbele au hatuwajali kwa kiasi kinachostahili.
Tunapaswa kuangalia namna gani watu wanaofanya shughuli hizi
wanakua rasmi kwa kupatiwa maeneo maalumu pamoja na utambulisho utakaowawezesha
kufanya kazi zao kwa Amani na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na si kama
walivyo sasa wanafanya kazi hizo katika maeneo yasiyo rasmi na kuhama kila siku
hali hii ina wafanya wajihisi kama si sehemu ya Taifa hili hivyo wanaweza
kutumika kiurahisi kuhatarisha amani ya Nchi yetu alisema Masangwa.
Akichangia katika viashiria vya uvunjifu wa amani Askofu
Dr. Leornard Mwizarubi wa Kanisa la SAYUNI EAG (T) alisema ni vyema
Serikali ikajikita katika kutatua changamoto zinazoathiri maisha ya kila siku
ya wananchi ili hata sisi viongozi wa dini tunapoongea na waumini tuwe na vielelezo
dhabiti vya kuonyesha namna ambavyo Serikali kero zao zimeshughulikiwa.
Aliendelea kusema “Katika eneo ambalo ninatoa
huduma ya Kiroho kwenye Kata za Unga Ltd, Sokoni 1, Daraja II, Sinoni na maeneo
ya jirani wakazi wa mitaa hiyo wanapata shida sana ya huduma ya maji Taka na
hata katika Kanisa langu inanilazimu kutafuta gari la kunyonya maji taka mara
tatu kwa wiki ili kufanya mazingira kuwa safi, sasa kuna maeneo mengine
wananchi hao hawana uwezo wa kutafuta gari hilo la kunyonya maji taka hivyo
wanaishia kulalamika kwa kuishi katika mazingira machafu”.
Aidha Sheikh Mkuu wa
Bakwata mkoa wa Arusha, Shabaan Juma alishukuru
Sekretariet ya Mkoa kwa kikao hiki muhimu kwa ustawi wa jamii ya Arusha na
kueleza kuwa katika kipindi hiki cha Mpito Nchi yetu inahitaji maombi ya bila
kikomo ili kuweza kuvuka salama na tunategemea kuendelea kuona mabadiliko
katika kila eneo; Tunaamini si wote
wanafurahia mabadiliko haya hivyo tuna wajibu wa kuwajulisha waumini
wetu kuhusu umuhimu wa mabadiliko ya mifumo katika uongozi wa Serikali ya Awamu
ya Tano na faida zitakazo patikana kwa Taifa.
Akiwasilisha
changamoto katika upande wake Sheikh Shaaban alisema “Kuna ukuaji wa kasi ya
makazi holela katika Jiji la Arusha,utaratibu wa mipango miji hauzingatiwi na
hii inasabisha maeneo mengi kutopitika kwa urahisi hivyo hata itakapotokea
dharua sio tahisi kwa wananchi wetu kupata msaada wa haraka, tunaomba wanachi
wapimiwe maeneo yao, barabara zifunguliwe ili huduma muhimu ziweze kufika
katika maeneo hayo”.
Mkurugenzi wa
Idara ya maji safi na maji Taka (AUWASA) Eng. Ruth Koya alisema Taasisi yake
inaanza utekelezaji wa Mradi mkubwa wa maji safi na Taka ambao matatizo yote
yaliyowasilishwa katika kikao hiki yanayohusiana na maji yatashughuliwa kupitia mradi huo.
Aliongeza kuwa
mradi huo utahusisha uboreshaji wa mioundombinu ya maji safi, Uhamishaji wa mabwawa
ya maji Taka(yaliyokuwa Lemara kwa hivi sasa), ununuzi wa magari ya kunyonyea
maji machafu pamoja na magari ya kusambaza na kuuza maji safi.
Mkuu wa Mkoa Mh.
Gambo alitolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na kuelezea namna
ambavyo Changamoto ya Mipango Miji ilivyopata ufumbuzi kupitia ukamilishaji
wa Mpango Mkakati wa Jiji la Arusha
(Master Plan) na kuwajulisha wajumbe kuwa mpango umekamilisha na umekwishapitiwa
na Halmashauri zote tatu zinazohusika, hivyo kwa hivi sasa utawasilishwa
Wizarani na taratibu zote zikikamilika utekelezaji utaanza mara moja.
Kuhusu suala la
Machinga na waendesha boda boda boda Rc Gambo alisema Serikali imekwisha anza
utaratibu wa kutafuta maeneo salama na rafiki
kwa ajili ya wafanyabishara ndogondogo maarufu kama machinga na
tutaongea nao ili tuwe na makubalino ya pamoja.
“Tumeanza
kuwatambua kupitia kwenye uongozi wa mitaa na vituo vyao na tutahakikisha
tunaboresha mazingira yoa ya kufanyia kazi na zaidi tunawatafutia Pikipiki ambazo watapewa Vijana wanaofanya
biashara ya boda boda kwa utaratibu maalumu; Itawapasa kurudisha Fedha za
Pikipiki tu na kisha kupata umiliki halali ya Chombo hicho tofauti na sasa hivi
ambapo wanapewa pikipiki hizo na kulipa mara mbili ya bei kwa matajiri wao
ndipo wapate umiliki,” alimalizia Gambo.

Post a Comment