Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi,
akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, alipofanya
ziara Jijini Mwanza hii leo.
Waziri
ameziagiza halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela mkoani
Mwanza, kuhakikisha zinakamilisha zoezi la upimaji na urasimishaji
makazi yaliyojengwa kiholela hadi ifikapo june 30 mwakani.
Na BMG
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi,
akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, alipofanya
ziara Jijini Mwanza hii leo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi,
akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi na makazi mmoja wa wakazi wa Kata
ya Buhongwa Jijini Mwanza ambaye makazi yake yamerasimishwa kutoka
makazi holela baada ya zoezi la upimaji kufanyika.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi,
akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi na makazi mmoja wa wakazi wa Kata
ya Buhongwa Jijini Mwanza ambaye makazi yake yamerasimishwa kutoka
makazi holela baada ya zoezi la upimaji kufanyika.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi,
akizungumza na watendaji mbalimbali Jijini Mwanza (Ilemela na
Nyamagana).
Baadhi ya Watendaji na Madiwani wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza
Baadhi ya Watendaji na Madiwani Jijini Mwanza
Pia
Waziri Lukuzi amempandisha cheo aliyekuwa Afisa Mipango na Maendeleo ya
Jiji la Mwanza, Deogratius Kalimerize, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mipango
Miji na Vijijini Kanda ya Ziwa.
Ni
baada ya kuridhishwa na kazi yake ya usimamiaji na uandaaji wa Mpango
Kabambe wa Jiji la Mwanza wa mwaka 2015-3015 ambao umelenga kulifanya
Jiji la Mwanza kuwa kitovu cha kiuchumi na biashara katika nchi za
maziwa makuu.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye mkutano huo baina
ya waziri Lukuvi na watendaji mbalimbali wa Jiji la Mwanza na Manispaa
ya Ilemela.
Watendaji na wananchi wa Kata ya Buhongwa wakimsikiliza waziri Lukuvi (hayupo pichani).
**********************
Na George Binagi-GB Pazzo
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, ameziagiza
halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza,
kuhakikisha zinakamilisha zoezi la upimaji na urasimishaji makazi
yaliyojengwa kiholela hadi ifikapo june 30 mwakani.
Waziri
Lukuvi ametoa agizo hilo hii leo Jijini Mwanza alikofanya ziara ya
kujionea utekelezaji wa urasimishaji makazi yaliyoendelezwa kiholela
Jijini Mwanza ambapo amebainisha kwamba Serikali haina mpango wa
kuwavunjia wananchi makazi yaliyojengwa kiholela na badala yake imeandaa
mpango huo ili kutambua makazi hayo na kuwapatia wananchi hati miliki
ya makazi yao.
Aidha
amewatahadharisha wananchi kwamba, mpango wa kurasimisha makazi
yaliyojengwa kiholela hautayahusisha makazi yaliyojengwa kwenye maeneo
hatarishi ikiwemo kwenye mabonde, miinuko, mafuriko pamoja na hifadhi za
barabara.
Baadhi
ya wananchi Jijini Mwanza ambao makazi yao yamerasimishwa na kupewa
hati ya umiliki, wameipongeza serikali kwa hatua hiyo ambapo wameomba
kasi ya zoezi hilo kuongezeka ili wananchi zaidi ya elfu 35 ambao makazi
yao hayajapimwa, yaweze kupimwa na kupatia hati za umiliki kwa wakati
kama Waziri Lukuvi alivyoagiza.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amemuhakikishia Waziri Lukuvi kwamba
hadi kufikia mwezi Januari mwaka ujao, zoezi la kupima makazi
yaliyojengwa kiholela na kuyarasimisha katika Jiji la Mwanza na Maspaa
ya Ilemela, litakuwa limekamilika.
No comments:
Post a Comment