Kupitia Ziara hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisikiliza kero za
wananchi wa eneo la soko Mjinga Kata ya Sokoni 1 ambapo kero kubwa ilikuwa ni
kufungwa kwa barabara kutokana na ujenzi holela
|
Kutoka Kulia ni Mhandishi wa Ujenzi Jiji Eng. Gaston Gasana
akifuatiwa na Mhandisi Mshauri wa Mradi wakielezea kazi zitakazofanyika katika
Mradi huu.
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo (kulia) akiskiliza taarifa ya kazi zinazoendelea katika Dampo la
kisasa la Muriet toka kwa Afisa Usafishaji wa Jiji Bw. James Lobikoki
|
Nteghenjwa
Hosseah - Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kuchunguza kwa undani juu ya zabuni aliyopewa
mkandarasi anaye jenga Barabara katika barabara ya Oljoro /Murriet Jijini
hapa.
Gambo ametoa agizo hilo wakati alipokuwa katika ziara ya siku moja
ya kukagua ujenzi wa Barabara ya Friends corner - Muriet inayojengwa Kwa kiwango cha Lami na mradi wa Mpango Miji Mkakati ( Tanzania Strategic Cities Project) unao tekeleza Na Tamisemi pamoja Barabara hiyo ya Oljoro - Muriet inayojengwa Kwa kiwango cha Changarawe kwa Fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Amesema amegundua kasoro Kwa Kampuni ya Surchet Building and Civil
works inayojenga Barabara ya Oljoro Kwa kuwa Mkandarasi yuko nyuma ya muda Na huenda asimalize kazi Kwa wakati. Pia dhamana ya Utekelezaji wa Mradi aliyoweka Ni kubwa kulinganisha na inayotakiwa hali hii inaonyesha kuwa zabuni hiyo ilitolewa Kwa mianya ya rushwa au dhamana hiyo Ni feki.
Kwa kawaida Dhamana ya Utekelezaji wa Mradi ( Perfomance bond) huwa Ni 10% Mpaka 15% ya Gharama ya Mradi lakin mkandarasi huyu amewasilisha 30% je dhamana hiyo ni halali kweli kwanini alete kiasi kikubwa zaidi ya kinachohitajika huenda Ni batili Ndio maana hana uchungu nayo na Mpaka sasa kazi iliyokamilika Ni ya ujenzi wa Mifereji tu sasa kupitia Ziara hii nahitaji uchunguzi wa kina ufanyike Na kazi hii ikamilike ndani ya muda wa mkataba alisema Gambo.
Barabara ya Oljoro Muriet inajengwa Kwa urefu wa Km 2.6 sambamba Na Mifereji ya kusafirishia maji yenye urefu km 1.1, Gharama Za Mradi Ni Tsh Mil 157.8 Na Barabara hii inategemewa kukamilika Mwishoni mwa Mwezi Oktoba 2016.
No comments:
Post a Comment