Mgombea urais Marekani wa chama cha Republican Donald Trump amekataa
kuahidi kukubali matokeo ya uchaguzi iwapo atashindwa, katika mjadala wa
mwisho wa urais dhidi ya Hillary Clinton.
"Nitakuambia wakati huo" alimwambia muendesha mjadala Chris Wallace. Kwa
siku kadhaa amedai kuwa kuna 'udanganyifu' katika uchaguzi huo.
Mjadala huo wa televisheni Las Vegas uliendeleza uhasama katika kampeni huku Trump akimuita Bo Clinton "mwanamke muovu".
Kura za kutafuta maoni zinaonyesha Trump poteza umaarufu katika majimbo
makuu baada ya kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono.
Mjadala huo wa mwisho wa umefanyika wiki tatu kabla ya siku ya uchaguzi Novemba 8.
Wagombea hao walikataa kusalimiana kwa mikono kabla na baada ya
majibizano hayo ya kisiasa, hatua iliyofungua kile ambacho baadaye
kiligeuka kuwa mjadala wa kelele na kukatizana kauli.
Trump alitoa ahadi kwa wanachama wa Republican kuwateua majaji wa
mahakama ya juu zaidi wanaoegemea 'mrengo wa kihafidhina' watakaogeuza
sheria kuu inayohalalisha uavyaji mimba Marekani na kulinda haki za
kumiliki bunduki.
Alisisitiza ahadi yake ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji ambao hawakusajiliwa na kudhibiti mipaka ya Marekani.
Wakati huo huo, Bi Clinton ametangaza wazi kuwa atawatetea wapenzi wa
jinsia moja, atalinda haki za kuavya mimba, atalenga kuinusha watu wa
kipato cha wastani na kushinikiza kulipwa sawa kwa wanawake.
"Serikali haina shughuli yoyote katika maamuzi wanayofanya wanawake," alisema.
Katika mojawapo ya nyakati zilizokuwa na mvuto, Trump alikataa mara
mbili kusema iwapo atakubali matokeo ya uchaguzi, hatua iliyobadili
utamaduni wa muda mrefu wa wagombea wanaoshindwa kukubali matokeo
baadaya kura kuhesabiwa.
"Hilo ni jambo la kuogofya," Clinton akajibu kwa ukali.
"Anaponda na kudharau demokrasia yetu. Na mimi kivyangu, nimeshangazwa
kuwa mtu ambaye ni mgombea mteule wa mojawapo wa vyama viwili vikuu
anaweza kuchukua msimamo wa aina hiyo."
Majibu ya Trump yamezusha shutuma kali kutoka kwa seneta wa Republican
Lindsey Graham, aliyesema mgombea huyo "hawajibi ipasavyo kwa chama
chake na taifa kwa kuendelea kuashiria kuwa anafanyiwa udanganyifu
katika uchaguzi ujao," kwa mujibu wa taarifa.
Kauli nyingine kuu katika mjadala katika chuo kikuu cha Nevada ni :
- Bi Clinton anasema Putin anataka Trump achaguliwe kwasababu anataka kinyago awe rais wa Marekani.
- "Tuna watu wabaya na tuta watoa," amesema Trump, aliposhinikiza ahadi yake ya kujenga ukuta mpakani.
- Bi Clinton amesema ataidhinisha mpango mkubwa wa ajira kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia.
- Trump ameashiria bi Clinto na rais Barack Obama walipanga ghasia katika mkutano wake wa kisiasa Chicago mapema mwaka huu.BBC
No comments:
Post a Comment