Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ili
kuzungumzia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Katika Mkutano huo Makonda amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele
katika kuhakikisha wanashiriki katika kupunguza au kuondoa kabisa
changamoto zinazowakabili ikiwemo, vibaka, dadapoa na uchafu wa
mazingira, akisema, ikiwa wananchi watashitiki kikamilifu ni rahisi
kukomesha tatizo la vibaka kwa sababu vibaka na dadapoa wanatoka
miongoni mwa familia zao na hali kadhalika uchafu wa mazingira unatokana
na takataka wanazozalisha wananchi wenyewe.
Viongozi
waandamizi katika Wilaya ya Ilala, wakimsikiliza mkuu wa mkoa Paul
Makonda wakati akihutubia wananchi katika eneo la Buguruni kwa Mnayamani . Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela
Palela, Ofisa Tawala wa Manispaa hiyo, Edward Mpogolo, Naibu Meya
Manispaa hiyo, Omary Kumbilamoto na Mbunge wa Segerea wilayani humo Bona
Kalua
Mjumbe
wa Shina namba tano, Katika Kata ya Myamani, Buguruni Zubeda Lugiga,
akieleza kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara.
Mkazi
wa Buguruni, Sadik Mgaya akieleza changamoto na kero zinazowakabili
wananchi wa eneo hilo wakati wa mkutano huo wa Makonda
Mkazi
wa Buguruni kwa Mnyamani, Samweli Ndyanabo, akieleza kero
zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda alipowahutubia katika mkutano wa hadhara jana jioni .
Kamanda
wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero
na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), uliofayika
Buguruni kwa Mnyamani
Kamanda
wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam, Simon Sillo akijibu hoja, kero
na changamoto mbalimbali walizouliza wananchi, katika mkutano wa mkuu wa
mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uliofayika Buguruni kwa
Mnyamani
Wananchi wakishangilia wakati hoja zao zikijibiwa na Kamanda Sillo
Wananchi wakishangilia wakati hoja zao zikijibiwa na Kamanda Sillo
Wananchi
wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, PaulMakonda wakati
akiwahutubia katika neo la Buguruni kwa Mnayamani
Ofisa
tawala wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, akimsikiliza
kwa karibu Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema, aliyekuwa akielezea
jambo,wakati wa mkutano wa hadhara wa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
uliofanyika leo Buguruni kwa Mnyamani Dar es Salaam. Katikati ni Mbunge
wa Segerea Bona Kalua
Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akitoa maelezo yake kuhusu
maswali waliyouliza wananchi, wakati wa mkutano wa Mkuu wa mkoa wa Dar
es Salaam, paul Makonda uliofanyika . Naibu Meya huyo
alizungumzia zaidi mradi wa Uwekezaji ulitaka kufanywa na kampuni ya PMM
katika eneo la mitaa ya Mnyamani na Kifaru, Buguruni, lakini mradi huo
umesimama.
Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipongezana na Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sillo mwishoni mwa mkutano
huo uliofanyika katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani.
Ofisa
Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ilala Msongela Palela wakifurahia jambo mwishoni mwa mkutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akifunga mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kwa kuendesha vizuri mkutano huo
Ofisa
Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edwars Mpogolo akimpongeza Mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda kwa mkutano kwenda vizuri
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akifurahiwa na Wananchi wakati
akiondoka baada ya mkutano wake wa hadhara aliofanya katika eneo la
Buguruni kwa Mnayamani, . Picha zote na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment