Mkurugenzi wa taasisi ya PWC Bi. Manda Ngoitiko (kushoto) pamoja
na Manger wa Kampuni ya Thompson
Safaris (kulia) kila mmoja akielezea namna ambavyo mgogoro wa ardhi uliopo
unavyoathiri shughuli zao za kila siku.
Nteghenjwa
Hosseah - Arusha
RC ARUSHA AKERWA NA HALI DUNI YA NGORONGORO
Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo mwishoni mwa wiki hii amekutana na wadau wa
taasisi zisizo za Kiserikali pamoja na makampuni yanayoendesha shughuli zao
katika Wilaya ya Ngorongoro lengo ikiwa ni
kusikia namna wadau hao wa maendeleo wanavyoendesha shughuli zao
halkadhalika Wilaya hiyo inavyonufaika
na uwepo wa wadau hao katika maeneo hayo.
Akizungumza wakati
wa kufungua Kikao hicho Rc Gambo alisema malego ya Kikao hiki yanaendana
sambamba na maandalizi ya Safari yake ya kikazi ya siku tano katika Wilaya ya
Ngorongoro itakayoanza tarehe 03-08/10/2016 hivyo angependa kufahamu kwa upana
namna ambavyo wadau hawa wanachangia katika kuleta maendeleo ya Wilaya hii
ambayo kwa kipindi kirefu imekua nyumba kimaendeleo.
Alisema sielewi
kwa nini kwa miaka yote hii Wilaya ya Ngorongoro haina hata kilomita moja ya
barabara ya Lami, Stendi ya Kisasa wala masoko yenye hadhi ya kuwahudumia
wageni ambao wengi wao ni watalaii wakati kuna taasisi za Kiserikali na siziso
za Kiserikali ambazo zina uwezo wa kutosha kuboresha huduma hizi kwa manufaa ya
wananchi na wageni wanaotembelea eneo hilo.
Wananchi wa
Ngorongoro wamekua na maisha duni na matatizo yasiyoisha, hakika sasa umefika
wakati wa kufahamu kazi zinazotekelezwa na
kila mdau na tufahamu kwanini uwepo wao hauchangii kulete mabadiliko
chanya katika Wilaya hii, huenda mipango kazi yao iko tofauti na malengo na
matarajio yetu hivyo tusije tukawalaumu kumbe ni kutofahamu namna ambavyo taasisi
zenu zinafanya kazi aliongeza.
“Katika Wilaya hii
ukizungumzia Taasisi kubwa za Serikali kuna Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro,
Baraza la wafugaji pamoja na Halmashauri ambao wanapata Fedha nyingi kwa ajili
ya kuleta maendeleo lakin bado kasi ya maendeleo kwa kweli hairidhishi kabisa,
ni vyema basi kwa pamoja tutafute majawabu ya matatizo yanayoikabili
Ngorongoro”, alisema Gambo.
Baada ya Taasisi
zote kuwasilisha taarifa zao iligundulika kwamba kuna mgogoro wa Ardhi ambao
sasa umekua wa muda mrefu kati ya Vijiji vya Sukenya, Soitsambu, Mondorosi na
Muwekezaji wa Kampuni ya Thompson.
Rc Gambo alisema
ni wakati sasa wa kuketi meza moja na makundi yote kuona namna ambavyo
tunaweza kutatua mgogoro huu ili
wananchi waweze kuendelea na shughuli zao na Muwekezaji afanye kazi zake kwa
amani katika eneo hilo na kupitia kikao hiki nimepata kufahamu vitu vingi
ambavyo ntakuja kuvifanyia kazi wakati wa Ziara yangu.
Ziara hii ya
Kikazi Wilayani Ngorongoro itakua ya pili tangu Mhe. Gambo alipochaguliwa kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema mwezi Agosti 2016.
|
No comments:
Post a Comment