Rais wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange leo tarehe 05 Oktoba, 2016
amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kurejea nchini
kwake.
Katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Kabila ameagwa
na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli.
Viongozi wengine
walioungana na Rais Magufuli wakati wa kumuaga Rais Kabila ni Makamu wa Rais
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa
vyombo vya ulinzi na usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda na
Viongozi wa Dini.
Katika
hatua nyingine, mara baada ya kuondoka kwa Rais
Kabila, Rais Magufuli amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya
kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal One ambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza
na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners)
zilikuwa hazifanyi kazi.
Mara hii Rais
Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye
mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.
Hata hivyo
amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha
kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili walitoa taarifa za uongo pindi alipofanya
ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.
"Leo kweli
mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya
kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua"
amesisitiza Dkt. Magufuli.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
05 Oktoba,
2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mara baada
ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kurejea DRC.
Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati
akipanda ndege kurejea nchini kwake mara baada ya kumaliza ziara yake
ya siku tatu hapa nchini
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja
na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakipunga mkono kuagana na Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila (hayupo pichani)
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Shekhe Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mara baada
ya kuagana na mgeni wake Rais wa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Joseph Kabila. kulia ni mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo Joseph Kabila katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) kabla ya kuondoka. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo Joseph Kabila wakati akimsindikiza katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kuondoka. Kushoto ni Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja
na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph
Kabila wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake wake Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakiangalia vikundi vya
ngoma za asili vilivyokuwa vikitoa burudani uwanjani hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Makamu wa Rais Samia Suluhu akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika
uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One kuangalia
ufanisi wa mashine hizo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Makamu wa Rais Samia Suluhu akiangalia ufanisi wa mashine za kukagulia
mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal
One na kukuta zinafanya kazi vizuri. Aliyekaa ni Mwendeshaji wa Mashine
hizo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege TAA-Grace Jonathan.
No comments:
Post a Comment