Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akizungumza na wajumbe
wa bodi ya utalii Tanzania(TTB) jijini Dar es Salaam leo wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa bodi ya utalii. Amesema kuwa bodi ya utalii
wanawajibu wa kutangaza vivutio vilivyopo hapa nchini ili kila mtu na
aweze kutembelea vivutio hivyo kwaajili ya kuongeza pato la Nchi.
Pia amesema kuwa Bodi ya Utalii inapaswa kulipa deni la bodi hiyo kwani linaleta doa katika bodi ya utalii hiyo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Utalii(TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na
wajumbe wa bodi ya utalii Tanzania jijini Dar es Salaam leo. Amesema
kuwa Bodi ya Utalii inakabiliwa na deni la shilingi bilioni 3.7 ambalo
limetokana na matangazo yaliyokuwa yakitangazwa nje ya nchi kwenye
viwanja vya mpira kwaajili ya kutangaza utalii.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Angeline Madete (Kulia )
na Mkurugenzi wa Wizara ya Maliasili na utalii, Zahoro Kimwaga wakiwa
kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Bodi ya Utalii Tanzania jijini Dar es
Salaam leo.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Utalii wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe jijini Dar es Saalaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe(Katikati) Mwenyekiti
wa Bodi ya Utalii(TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kushoto na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Angeline Madete wakiwa
katika picha ya Pamoja na wajumbe wa bodi ya Utalii (TTB)jijini Dar es
Salaam leo.
No comments:
Post a Comment