Pages

August 23, 2016

VIJANA WA CCM KUFANYA MAANDAMANO NCHI NZIMA AUGOSTI 31 MWAKA HUU

Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) , Shaka Hamdu Shaka .
Dar es Salaam. Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imepanga kuitisha maandamano nchini nzima Agosti 31 mwaka huu yenye lengo kumpongeza Rais John Magufuli kutokana utendaji kazi tangu aingie madarakani.

Kaimu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Shaka Hamdu Shaka alisema maandamano hayo ni ya amani tofauti na vyama vingine na tayari wameshatoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya ulinzi.


Alisema Rais Magufuli amefanya mambo mengi katika kipindi kifupi alichokuwa madarakani hivyo hawana budi kumpongeza kwa njia ya maandamo ili kufikisha ujumbe kwa wananchi waliomchagua.MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...