Pages

August 22, 2016

Samatta kaipatia ushindi mwingine timu yake ya KRC Genk

Baada ya mtanzania Mbwana Samatta kuingoza timu yake ya KRC Genk kicheza mchezo wa kwanza wa round ya mwisho wa kuwania kufuzu hatu ya Makundi ya UEFA Europa League dhidi ya Lokomotiva ya Croatia na mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.    
August 21 2016 alishuka dimbani    kucheza mchezo wao wa nne wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Lokeren katika uwanja wa Diknam unaotumiwa na Lokeren kama uwanja wa nyumbani.    
Leo August  21 Samatta amefanikiwa kuiongoza Genk kuibuka na ushindi  wa goli 3-0 huku Samatta akifanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 34 na 38 kabla ya mjamaica Leon Bailey kufunga goli la mwisho dakika ya 48, Genk sasa inakuwa inafikisha jumla ya point 7 na kuwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi kuu Ubelgiji.
Wakatii huu mtanzania Mbwana Samatta akiwa kafikisha jumla ya goli tatu katika michezo yao minne ya Ligi Kuu waliyocheza msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...