Pages

August 1, 2016

ESRF YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUICHAMBUA BAJETI YA SERIKALI KATIKA SETA YA AFYA NA VIWANDA

TAASISI ya Utafiti ya Uchumi na Jamii (ESRF) imewakutanisha wasomi na wawakilishi wa taasisi za umma na kibinafsi kuchambua bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Sekta ya Afya na Viwanda ili kuona inavyoweza kutatua changamoto zinazokabili Sekta hizo kwenye mdahalo uliokutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi na kufanyika makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Akifungua mdahalo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt.Tausi Kida alisema, Taasisi yake imeona ni vema kuwakutanisha wadau kujadili bajeti hiyo katika sekta ya Afya na Viwanda, kwa vile zinagusa uchumi wa wananchi.

Akiwasilisha mada juu ya bajeti ya Serikali 2016/2017na changamoto zinazoikabili sekta ya Afya, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi, Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja alisema, ingawa bajeti iliyotengwa kwenye sekta ya Afya ni kubwa, lakini bado kuna changamoto kadhaa kwa vile Wizara hiyo imepanuka kutokana na kuhudumia maeneo mengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mdahalo uliolenga kujadili changamoto zinazoikabili bajeti ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Afya na Viwanda, kwenye makao makuu ya ESRF jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo umewakutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said).

Profesa Mujinja alitolea mfano wa ununuzi wa madawa ambapo, zaidi ya asilimia 90 ya madawa yanayotumika huagizwa kutoka nje na hivyo fedha nyingi za kigeni hutumika.

Katika majumuisho yake, Profesa Mujinja alisema, ni vema Serikali ielekeze nguvu zake kwenye uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha madawa na vifaa tiba hapa nchini ili kwenda sambamba na malengo ya taifa ya maendeleo endelevu.

Akizungumzia kuhusu changamoto za bajeti kwenye eneo la Viwanda, muwasilisha mada Profesa Prosper H. Ngowi kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, alisema, fedha zilizotengwa kwenye Sekta ya Viwanda ni Shilingi Bilioni 81, 871,992,000, ambapo asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na asilimia 49 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Kwa mtazamo wake, Profesa Ngowi alisema, mgawanyo huo ni mzuri na sio kwa kiwango kikubwa kwani hakuna tofauti na bajeti ya mwaka 2015/2016, na kuonyesha wasiwasi wake muda ambao Serikali inatoa fedha hizo kuhudumia maeneo yaliyokusudiwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Cha Muhimbili, Profesa Phares Mujinja, akitoa mada juu ya changamoto zinazoikabili bajeti ya Serikali ya 2016/2017 kwenye Sekta ya Afya wakati wa mdahalo huo.

“Bajeti ya 2016/2017 ni Asilimia 70.3% ya ile ya 2015/2016 na kwamba wizara hivi sasa ni kubwa kutokana na kuongezeka kwa sekta ya Uwekezaji.” Alifafanua.

Wakichangia mada hizo, wengi wa washiriki wameonyesha wasiwasi wao kuhusu kufanikiwa kwa malengo ya serikali kwenye Sekta hizo kutokana na muonekano wa bajeti yenyewe na mahitaji halisi ya sasa ya utoaji huduma kwenye Sekta hizo ili kufikia malengo ya kukuza uchumi wa nchi kumekuwepo kwa mtazamo kuwa biashara nchini zinaanguka kutokana na mkazo wa kukusanya mapato.

Akifunga mdahalo huo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Ujenzi wa Maendeleo wa ESRF, Doris Likwelile, aliwashukuru washiriki kwa michango yao mbalimbali na kwamba mawazo yao yatawezesha utayarishaji wa mtazamo wa wadau kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 kwenye Sekta hizo mbili za Afya na Viwanda.
Edith Mackenzie, akichangia kwenye mdahalo huo.
Mkuu wa Program ya Taarifa na Utafiti kutoka TGNP, Gloria Shechambo akishiriki kwenye mdahalo huo.
Mkurugenzi wa SIKIKA, Irinei Kiria, akichangia mawazo yake kwenye majadiliano hayo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Prosper Ngowi, akiwasilisha mada ya changamoto zinazoikabili bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Viwanda hapa nchini, wakati wa majadiliano yaliyowaleta pamoja wasomi na wawakilishi wa taasisi za Umma na Binafsi kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Majadiliano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF).
Dkt. Kida akichangia baadhi ya hoja za washiriki na watoa mada. Kushoto ni Profesa Prosper Ngowi.
Baadhi ya washiriki wa majadiliano hayo.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Ujenzi wa Maendeleo wa ESRF, Doris Likwelile, akitoa hotuba ya kufunga mdahalo huo.
Afisa Mpipango Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, (TPA), Alfred Matuntera, (kushoto0, akizungumza jambo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida, (kulia), Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Afya Shirikishi Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja, (wa pili kulia), na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Prosper Ngowi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...