Pages

July 25, 2016

WATANZANIA WAASWA KUWA WAZALENDO NA NCHI YAO




Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Christina Mndeme akiwasha Mwenge wa uhuru katika mnara wa mashujaa kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mshujaa, hafla iliyofanyika Saa Sita Kamili usiku ya tarehe 25 julai 2016 Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Jordan Rugimbana akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuupa heshima Mkoa wa Dodoma wa kuadhimisha siku ya mashujaa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge na kutoa rai kwa watanzania kuwa wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya mtu kama walivyofanya wazee wetu waliopigania uhuru wa nchi.

Wanajeshi wa Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwashwa kwa Mwenge kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mshujaa yatakayofanyika tarehe 25 julai 2016 Mkoani Dodoma.

Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Serikali wakishuhudia uwashwaji wa Mwenge.

Mwenge wa uhuru mara baada ya kuwashwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Christina Mndeme, Tarehe 25 julai 2016 Saa Sita Kamili usiku Mkoani Dodoma. PICHA NA HASSAN SILAYO


Na. Immaculate Makilika Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama amesema kuwa kufanyika kwa maombolezo ya kumbukumbu za Mashujaa inawakumbusha watanzania kuwa wazalendo.

Akizungumza wakati wa maombolezo ya kumbukumbu za Mashujaa sambamba na kuwashwa kwa Mwenge wa Uhuru katika mnara wa kumbukumbu za Mashujaa, leo usiku katika viwanja wa Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma, Waziri Mhagama alisema kuwa kufanyika kwa maombolezo ya Mashujaa mkoani Dodoma ni heshima kwa wananchi wa Dodoma na watanzania wote kwa ujumla.

“Kufanyika kwa maombolezo haya inatukumbusha watanzania kuwa wazalendo na kupigania bila kuchoka, bila kujali makabila yetu na tujifunze kwa Mashujaa hawa waliopigania uhuru wetu” alisema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama aliwaomba watanzania kutumia siku ya kumbukumbu ya Mashujaa ambayo ni Julai 25, kwa namna mbalimbali ikiwemo kufanya maombi ya sala kwa Mashujaa wote walifariki katika harakati mbalimbali za kupigania uhuru wa Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimwa Jordan Rugimbana aliishukuru Serikali kwa uwamuzi wa kuadhimisha kumbukumbu za mwaka huu za Mashujaa mkoani Dodoma, na kusema kuwa kufanyika kwa tukio hilo la kihistoria linakumbusha uwajibu wa watanzania na Mkoa wa Dodoma utaienzi heshima hiyo.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mheshimiwa Christina Mndeme aliwasha Mwenge wa Uhuru katika kilele cha mnara wa mashujaa mnano saa 6 kamili usiku ikiwa ni sehemu ya maombolezo ya kumbukumbu ya Mashujaa.

Mnara wa Mashujaa uliopo mkoani Dodoma ni kati ya vituo 4 vilivyopo nchi nzima ambavyo vimekuwa na makaburi ya Mashujaa mbalimbali waliopigania uhuru wa nchi ya Tanzania. Vituo vingine vipo meneo ya Mtwara, Dar es Salaam na Kagera.

Maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kesho julai 25, mkoni Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...