Na Leonard Msigwa/GPL
Rais
Salva Kiir wa Sudan Kusini ameitwa na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta
Museveni kwenye Ikulu ya nchi hiyo na kufanya mazungumzo naye.Ziara hiyo
ya ghafla imekuja siku chache baada ya kutokea kwa mapigano makali
kwenye mji wa Juba ambao ndiyo makao makuu ya nchi ya Sudan
Kusini.Mapigano hayo yalivihusisha vikosi vitiifu kwa Rais Kiir dhidi ya
vile vinavyomuunga mkono Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Riek Machar
ambaye mpaka sasa hajulikani wapi alipo tangu kuzuka kwa mapigano
hayo.Lengo la ziara hiyo ya ghafla ni kujaribu kutatua mgogoro baina ya
Rais Kiiir dhidi ya makamu wake na baada ya mazungumzo hayo Rais Kiir
amerejea nchini kwake.
No comments:
Post a Comment