Na Mchambuzi wetu Geofrey Chambua.
Jana
ziliripotiwa taarifa kupitia BBC kwamba ndege za kivita za Israeli
zimetekeleza msururu wa mashambulizi ya asubuhi mapema huko Gaza
Likishambulia maeneo manne yanayohusishwa na wapiganaji wa Hamas.
Huenda ni vyema kuutumia wasaa huu kujuzana KWA KINA NA VINA kuhusu hali halisi ya Ukanda huu wa Gaza
Ukanda wa Gaza (Strong City) ni eneo dogo kwenye mwabao wa Mediteranea ya Mashariki lililopo sehemu ya mamlaka ya Palestina. Lina urefu wa kilomita 40 na upana kati ya 6 km na 14 km. Eneo lote halizidi 360 km².
Ni kati ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu likiwa na wakazi
milioni 1.4 na ni moja ya nchi zinazoongoza kwa msongamano duniani (the
most crowded on earth)
Kanda hili ni kati ya mabaki ya Palestina ya Kiingereza yasiyotwaliwa na Israel wakati wa vita ya Kiarabu-Kisraeli ya 1948 na kuwa kimbilio kwa wakimbizi wengi Wapalestina waliowahi kukaa katika sehemu zilizokuwa Israel
1.
Gaza imezungukwa katika pande zake zote tatu na Israel ambao wameblock
pande hizo zote tatu kwa kutumia jeshi lao la anga na jeshi la majini.
Upande wa nne ni borderpoint ya Egypt ambapo jeshi la Misri pamoja na
majeshi ya Israeli na lile la wasimamizi wa UN na walinda amani
wamefunga njia hizo na yeyote haruhusiwi kutoka ama kuingia ndani ya
Gaza.
2.
Gaza ni kama gereza kubwa sana ambapo huenda hata sisimizi hana ruhusa
ya kuweza kutoka ama kuingia humo bila ruhusa ya Israel. Hii ni kwa
sababu wanamgambo Wapalestina maarufu kama HAMAS ambao ndio wanaoongoza
Serikali ya nchi hiyo, wanaendelea kurusha roketi ndogo kutoka Gaza
kwenda Israel.
3. Gaza haina kiwanja cha ndege, bandari wala hata japo kituo cha treni.
4.
Wakazi wa Gaza hawawezi kuondoka nchini mwao kwenda mahali popote kwa
kuwa hawana passport . Pia kuna vituo vya ukaguzi vya Israeli kila
mahali. Pili hakuna mtu yeyote toka nchi yeyote anayeweza kuingia Gaza
pasipokuwa na kibali maalumu ama ruhusa toka kwa serikali ya Israel
ambayo hata hivyo pia ni ngumu sana kuipata ruhusa hiyo. Hii pia
inawahusu wanasiasa nguli duniani kuingia Gaza ni mbinde. Hata David
Cameroon aliwahi kuifananisha Gaza na ‘Kambi ya Wafungwa’ (Prison Camp)
5.
Gaza ni sehemu ambayo kiujumla imetenganishwa mbali sana na sehemu
kubwa ya nchi zingine za dunia hii haya yamefanywa na israel. Kila siku
inayopita bidhaa zote zinazotumika kwa mahitaji ya watu wa Gaza ni
lazima zipitie katika vituo vya ukaguzi vya Israeli. Hata
maziwa,ngano,madawa na bidhaa zote hupitishwa kwanza katika check point
za Israel. Israel hutoza kodi kwa bidhaa zote hizi zinazopita katika
vituo vyao vya ukaguzi kwenda Gaza
6.
Umoja wa Mataifa UN umewasihi mara kadhaa serikali ya Israel kuondoa
vizingiti hivyo na mamlaka yake ndani ya Gaza Israel imekuwa kama sikio
la kufa haisikii. Zaidi ya maazimio 50 yamepitishwa na UN dhidi ya
Israel lakini Israel hawajali wala kusikiliza.
7.
Vyakula na mahitaji muhimu daima huwa haba kutokana na uingizwaji wa
kiwango kidogo mjini Gaza kwa kuwa Israel huchelewesha kwa makusudi,
wanahujumu na kuzuia uingizwaji wa bidhaa hizo Gaza. Maduka hayana
bidhaa,hospitali hazina madawa muhimu .
8.
Nishati ya umeme ipo kwa uchache sana bidhaa kama petrol na gesi
upatikanaji wake pia ni mgumu sana pia . Kiwango cha mfumuko wa bei ni
kikubwa kuliko mahala popote duniani kutokana na vitendo vya Israel.
Umasikini nao umezidi kuinuka kupita maelezo. Watoto wa Gaza kwa sasa
nao wamo katika orodha ya watoto wanaogua utapiamlo kwa kiwango kikubwa
duniani kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
9.
Hakuna madaktari maalumu au vifaa muhimu vya kutibia majeraha makubwa
au hata madawa katika hospital nyingi. Wakati huo kila saa inayopita
jeshi la Israeli hurusha makombora kuelekea Gaza na raia wasio na hatia
hupata majeraha na kuumizwa vibaya na mabomu hayo huku wakikataliwa
kwenda kupata matibabu nje na jeshi la Israeli. Hivyo majeraha haya
ambayo yangeweza kutibika hushindwa kupata tiba na matokeo yake hugeuka
sugu na baadaye kuwa ni ulemavu wanaoishi nao maisha yao yote.
10.
Jamii hii ya Gaza ambayo hapo nyuma ilikuwa yenye hali nzuri kimaisha
na utajiri kwa sasa imegeuka na kuwa omba omba na wafungwa ndani ya nchi
yao wenyewe .Unaweza kuhisi maumivu ya miili yao,
ukandamizaji,udhalilishaji,maumivu ya mioyo ya watu hawa waliovamiwa na
kufanywa watumwa na wafungwa ndani ya nchi yao? Kwa Mujibu wa Shirika la
Takwimu la Gaza, ni asilimia 28 tu ya wakazi wa Gaza wenye ajira huku
vijana wakiwa ni 58% KATI YAO
11.
Wamepigania uhuru wao zaidi ya miaka karibia 50 sasa lakini Kila siku
inavyopita matumaini yao ya uhuru yanazidi kufifia. Kuelekea mazungumzo
ya kutafuta amani, Israel haipo tayari inataka kuchelewesha uhuru wao
ili kuzidi kuchukua ardhi yao zaidi kila siku kwa kujenga makazi mapya
na nyumba za waisrael. Gaza iko chini ya serikali ya Hamas lakini maeneo
mengine yako chini ya mamlaka ya Rais Mahmoud Abas.
Yasemekana
Vyombo vya habari vya magharibi vimelipwa na kutengeneza habari ambazo
zinaweza kuonyesha dunia kama vile wakazi wa Gaza ndio ambao wamevamia
ardhi ya israel na hivyo basi Israel wanapigania uhuru wao toka kwenye
uvamizi wa Gaza!!
No comments:
Post a Comment