Baada
ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za
kimataifa , timu ya soka ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
‘Serengeti Boys’, imebakiza mitihani miwili kabla ya kuandika historia
ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, imefahamika.
Mtihani
wa kwanza ni mchezo dhidi ya Afrika Kusini unaotarajiwa kufanyika ama
Agosti 5, 6 au 7, 2016 ambako mechi ya kwanza itapigwa ugenini kabla ya
kurudiana jijini Dar es Salaam, Tanzania wiki moja baada ya mchezo huo.
Hivyo mchezo wa marudiano utafanyika Uwanja wa Azam Complex, ulioko
Chamzi Agosti 14, 2016 saa 9.00 alasiri.
Mshindi
wa jumla katika michezo hiyo, itacheza na timu mshindi kati ya Namibia
na Congo-Brazaville. Wakati Afrika Kusini imepitishwa moja kwa moja
Namibia imepenya kwa kuiondoa Botswana licha ya kufungwa mabao 2-1
katika mchezo wake uliofanyika jana Julai 2, 2016 huko Botswana.
Katika
mchezo wa kwanza uliofanyika Namibia, Juni 24, mwaka huu wenyeji
(Namibia) walishinda 1-0. Kwa msingi huo, Namibia imepenya kwa bao la
ugenini ililolivuna katika mchezo wa jana. Bao la ugenini imefanya kuwa
na mabao 3-2.
Kocha
Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo Shime, ameangalia ratiba ya
mlolongo huo na kusema “Ushindani utakuwa mkubwa, lakini mimi nimelenga
kushinda michezo yote iliyo mbele yangu. Si kwamba napigania kufuzu
kwenda Madagascar tu kwenye fainali za Afrika, la hasha, nataka timu hii
niipeleke Kombe la Dunia.”
Fainali
za Kombe la Dunia, mwakani zitapigwa India ambako kama Serengeti Boys
itafuzu kucheza fainali za Afrika na ikaingia nusu fainali kwa maana
timu nne bora zote zitashiriki fainali hizo ambazo tayari Tanzania
imejiwekea mazingira mazuri ya kufuzu.
“Timu
hii nimeanza nayo zaidi ya mwaka mmoja. Sioni kama itakuwa kikwazo
kuifanikisha kufika fainali za Kombe la Dunia. Namuomba Mungu
atunyooshee mkono wake, nawaombea viongozi wa TFF wazidi kuihudumia timu
hii, lakini pia wadau wengine waisapoti timu hii bila kuangalia au
kuchagua mtu anayeongoza TFF. Hii ni timu ya Watanzania wote,” amesema
Shime maarufu kama Mchawi Mweusi.
Shime
alishukuru mipango na ahadi ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kugharamia kambi ya wiki mbili
itakayofanyika Madagascar kuanzia Julai 24, mwaka huu akisema: “Hii
itakuwa ni kambi bora. Kwa sasa kikosi change kinahitaji utulivu hivyo
kwa maoni na mipango yangu naona inafaa.”
Naye,
Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu kwa Vijana anayeongoza timu
hiyo, Ayoub Nyenzi kadhalika aliomba sapoti ya Watanzania ili kuendeleza
timu hiyo, amesema: “Hakika nikipata watu wakatusapoti, naamini ndoto
zangu zitatimia .”
Nyenzi
amethibitisha kwamba timu hiyo itaondoka hapa jijini Victoria kesho
Jumatatu Julai 4, 2016 saa 11.00 jioni Kisiwa cha Mahe miongoni mwa
visiwa 115 vya nchi hii ya Shelisheli na inatarajiwa kufika Tanzania saa
7.45 usiku wa kuamkia Jumanne Julai 5, mwaka huu.
“Wachezaji
watakuwa na mapumziko mafupi kabla ya kuanza kambi ya maandalizi kwenda
Madagascar kwenye kambi ya kuiandaa timu kucheza na Afrika Kusini,”
amesema Nyenzi ambaye pia alijibu kuwa watawapumisha nyota hao kwa
ushauri wa makocha na daktari: “Mapumziko mafupi. Msihofu”
Timu
hiyo yenye wachezaji 20 na viongozi wanane, itasafiri kwa ndege ya
Shirika la Ndege la Ethiopia hadi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kubadili ndege ya kuunganisha kwenda Dar
es Salaam, Tanzania. Ikiwa Shelisheli ilifikia hoteli ya Berjaya Beau
Vallon Resort, iliyoko jijini Victoria. Hoteli ipo umbali wa Kilometa 25
kutoka uwanja wa ndege.
Nyota
waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili na Samwel Edward
Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement
Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein
Msengi, Issa Abdi Makamba.
Viungo
ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali,
Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Yassin Muhidini
Mohamed, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Rashid Mohammed
Chambo, Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola, Muhsin Malima
Makame Vitalis.
Hivi
karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki
mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF
International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya
kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
No comments:
Post a Comment