Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan
Kolimba (Mb.), akizungumza katika maadhimisho ya Miaka 59 ya Kiongozi
Mkuu wa Madhehebu ya Shia Ismailia, Mtukufu Aga Khan tangu aliposhika
nafasi hiyo.Katika hotuba yake Dkt. Kolimba alitumia nafasi hiyo
kumpongeza Mtukufu Aga khan kwa mafanikio katika kipindi cha uongozi
wake na kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali
ya maendeleo iliyochini ya Taasisi yake. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa
Ismailia hapa nchini, Bw. Amin Kurji.
Mkurugenzi
wa masuala ya kidiplomasia katika Taasisi ya Aga Khan, Balozi Arif
Lalani pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza
Mhe. Kolimba (hayupo pichani) alipokuwa akiendelea kuzungumza kwenye
maadhimisho hayo.
Katibu
wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara(Kulia) akifuatilia hotuba ya Mhe.
Kolimba pamoja na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Bi. Hellen Mgeta.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Ramla Khamis (wa
pili kutoka kushoto), akiwa pamoja na Maafisa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa hafla hiyo.
Sehemu
ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo nao wakimsikiliza Dkt.
Kolimba, wa pili kutoka kulia ni Balozi wa Japan hapa nchini Mhe.
Masaharu Yoshinda.
Wageni waalikwa .
Mhe.
Dkt. Kolimba na Bw. Kurji wakiwatakia afya njema Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mtukufu Aga Khan
wakati wa hafla hiyo.
Dkt. Kolimba akitambulishwa kwa wageni waalikwa na Bw. Kurji
Dkt.
Susan Kolimba akipokea maelezo kutoka kwa mtaalam aliyebuni mchoro waa
Chuo Kikuu cha Aga Khan kitakachojengwa Jijini Arusha.
Picha na Reginald Philip
No comments:
Post a Comment