Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu
wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada
ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki
hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali kiasi cha
shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kulia), akiwa
katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (kushoto), Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) na Mwakilishi Mkazi
wa AfDB, Tania Kandiero (wa tatu kushoto), baada ya kumalizika kwa
mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi
kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.Picha Zote na Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), akipeana mkono na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika -AfDB, Tania Kandiero,
alipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, kwa
mazungumzo maalumu, akiwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic
Kacou, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa
serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto), akimsikiliza kwa makini Makamu
wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia)
ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali
mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn. Aliyeketi kushoto ni Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Kushoto) akibadilishana "Business Card" na Makamu
wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada
ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki
hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka
2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akifuatilia kwa
makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,
Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia
Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi
433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), (Katikati), akiwa
katika mazungumzo maalumu na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi yake
Jijini Dar es slaam, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa
Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
Kaimu
Kamisha Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta
Mtagwaba akifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani), ambapo
Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka
2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akibadilishana "Business Card" na Makamu
wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada
ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki
hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka
2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa katika mazungumzo
maalumu na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ukiongozwa
na Makamu
wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou, aliyeambatana na Mkurugenzi
Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero, ambapo Benki hiyo
imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017,
kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto)
akizungumza jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo
ya Afrika-AfDB, ukiongozwa na Makamu
wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia)
ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali
mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Na Benny Mwaipaja-WFM
BENKI ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, imeahidi kuchangia Dola Milioni
200, sawa na Shilingi 433.6b, kwenye Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali
katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2016/2017.
Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anayeshughulikia
Utawala na Rasilimali watu, Dkt. Alberic Kacou, alipomtembelea Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Ofisini Kwake Jijini Dar es
salaam
Makamu huyo wa Rais wa AfDB aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa
Benki hiyo, Tania Kandiero, amesema kuwa mchango huo umeongezeka kwa
dola Milioni 50 ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka jana ambapo Benki hiyo
ilichangia Dola Milioni 150. "Misaada na mikopo inayotolewa na Benki
yetu kwa serikali ya Tanzania imefikia Dola za Marekani 1.9b hivi sasa"
Alieleza Dkt. Kacou
Ameeleza kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza katika Bara la Afrika
kupewa kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mipango yake mahili ya
maendeleo inayokidhi vigezo na viwango vya taasisi hiyo. "Tuna malengo
matano ambapo tunataka kuwekeza katika sekta ya nishati, uzalishaji wa
chakula, kuiendeleza kiviwanda, kuiunganisha na kuboresha maisha ya
waafrika kwa ujumla" aliongeza Dkt. Kacou
Amepongeza jitihada zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, kwa kusimamia vizuri nidhamu ya
matumizi ya fedha za umma na kwamba uamuzi huo utaharakisha maendeleo
ya nchi. Akizungumza na ujumbe huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Mpango, ameshukuru uamuzi wa Benki hiyo wa kuongeza mchango wake
katika Bajeti Kuu ya serikali kupitia mfuko mkuu wa Bajeti (GBS).
Amesema kuwa serikali imedhamiria kutekeleza mipango yake ya ujenzi
wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge), pamoja na
kununua ngege tatu za abiria ili kuboresha usafiri wa anga.
"Vilevile tumeamua katika Bajeti ya mwaka huu kununua meli mpya
itakayo tumika kutoa huduma Ziwa Viktoria na kukarabati meli nyingine
mbili ambapo moja iko Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Viktoria ili
kuimarisha usafiri wa majini" Aliongeza Dkt. Mpango
Dkt. Mpango amebainisha kuwa katika kutekeleza Mpango wa Pili wa
Taifa wa Maendeleo, serikali imejipanga kukuza sekta ya viwanda ili
kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. "Mpango huo
utakwenda sambamba na kuboresha sekta ya kilimo ili malighafi
itakayozalishwa na wakulima, licha ya kuinua uchumi wa wakulima wetu,
lakini pia viwanda vitapata malighafi ya kutosha" alisisitiza Dkt.
Mpango
Amerejea msimamo wa serikali kuwa haitakubali kupokea misaada
inayoambatana na masharti magumu na isiyo na tija kwa nchi na kwamba
jitihada zinazofanyika hivi sasa ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo
nchini zinawekezwa kwa utaratibu mzuri ili ziweze kutumika kuleta
maendeleo.
"Hatutakubali misaada isiyozingatia vipaumbele vyetu na ile
inayohatarisha uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu wenyewe" alieleza
Dkt. Mpango.Ameeleza kuwa uamuzi wa serikali wa kukusanya mapato yake ya
ndani kwa kuwahimiza watu kulipa kodi na kubana matumizi yasiyo ya
lazima umeanza kuleta matunda na kuongeza pia nidhamu ya matumizi ya
pesa katika jamii.
Ameiahidi Benki hiyo ya maendeleo ya Afrika-AfDB, kwamba fedha waliazoahidi kuzitoa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment