Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameviagiza viwanda vyote nchini kutumia msibomilia (BARCODES) za Tanzania kama hatua ya kuimarisha masoko na utambulisho wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na ya nje ya nchini.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa kampeni ya “NUNUA 620 Nunua Bidhaa za Tanzania” pamoja na Kusherekea miaka MITANO ya Taasisi ya Global Standard One –GSI-kwenye Viwanja wa Mwalimu Nyerere katika Maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (SABASABA) mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho.
Makamu
wa Rais amesema matumizi ya BARCODES ni muhimu na ni ya lazima kwa
sababu yanajumuisha taarifa nyingi ikiwemo asili ya bidhaa,jina la
kampuni, kumbukumbu za uzalishaji,utunzaji,usafirishaji na usambazaji wa
bidhaa.
Ameleeza kwamba itakuwa ni aibu kubwa kama katika masoko ya ndani ya nchi bado kutakuwa na bidhaa zinazotumia msibomilia (BARCODES) za nje na kusisitiza kuwa matumizi ya Barcodes za Tanzania zitazuia na kupungua upotevu wa ajira kwa wataalamu wa ndani ya nchi.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali ya awamu ya TANO ipo
Tayari kufanya kazi na sekta binafsi katika kuleta mapinduzi makubwa
yatakayosaidia kukuza uchumi wa Taifa.
Kuhusu uanzishwaji wa Majukwa ya kumwezesha wanawake Kiuchumi nchini,
Makamu wa Rais amesema kuwa atahakikisha majukwaa hayo yanaleta matokeo
chanya na yenye tija kwa wanawake Wakitanzania mijini na viijijini kwa
kuwezeshwa kupata kupata elimu ya ujasiriamali,fursa za
masoko,upatikanaji wa mikopo nafuu pamoja na elimu ya kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazowakwaza wanawake kiuchumi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizindua kampeni ya NUNUA 620 (msibomilia)
katika ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wengine pichani ni Mwenyekiti wa
Bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara na Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kushoto) kwenye maonyesho ya biashara ya
kimataifa jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye bango la GS1 mara baada ya kuzindua
kampeni ya NUNUA 620 kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatma Kange .
Wanawake
kutoka Majukwaa mbali mbali ya Wanawake nchini wakishangilia kwa
kujumuika na Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan (katikati) baada ya kuzindua kampeni ya NUNUA 620
kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa wakati maonyesho ya 40 ya Biashara
ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijage wakati wa kutembelea maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa
maarufu kama Sabasaba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia moja ya jiko lililotengenezwa Tanzania na rafiki wa
mazingira wakati alipotembelea mabanda mabali mbali kwenye maonyesho ya
40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia kabati lililotengenezwa kwa mbao ya mnazi wakati
alipotembelea moja la banda la wajasiriamali kuotoka Zanzibar wakati wa
maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba jijini
Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumzana fundi wa kushona nguo mwenye ulemavu wa macho (asiyeona)
ambaye anafahamika kama Mtaalamu wa kushona Tanzania Ndugu Abdallah
Nyangalio, kulia ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijage wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es
salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangali moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wanawake
wakati wa maonyesho ya kimataifa ya biashara
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia ubunifu wa hali ya juu ya gauni la kanga kwenye moja ya
mabanda ya wajasiamali wa Kitanzania wakati wa maonyesho ya 40 ya
Biashara ya Kimataifa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiongozana na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna
Mkapa
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipewa maelezo juu ya bidhaa zinazotengenezwa nchini na Bi. Flaviana
Tesha wa Kampuni ya Chai Bora wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya
Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiuliza maswali mbali mbali alipotembelea banda la Benki ya Watu wa
Zanzibar kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment