Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki
ya mazingira duniani ambapo manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na
Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd na nyingine kwa kufanya usafi
katika fukwe za bahari ya Salender jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni na
kulia ni Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw.
Abdon Mapunda.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni akizungumza jambo
na wadau wa mazingira waliokusanyika kwenye viwanja vya Salender Club
kabla ya kuanza zoezi la usafi wa mazingira.
Baadhi
ya wadau wa mazingira kutoka ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,
makapuni ya usafi yaliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala
ikiwemo Green Waste Pro Ltd, Vijana kutoka Roots and Shoot
waliokusanyika kwenye uzinduzi wa wiki ya mazingira duniani
iliyozinduliwa jana duniani kote.
Kiongozi
wa dhehebu la Dawoodi Bohra nchini, Bw. Zainuddin Adamjee (wa pili
kushoto) akimtambulisha Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra
duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin (wa tatu kushoto)
kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) mara baada ya
kuwasili jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Waziri wa Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph
Sokoine (kushoto) akitoa salamu za serikali kwa Kiongozi Mkuu wa dhehebu
la Bohora duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin
aliyewasili jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akielezea mipango ya manispaa ya Ilala
katika kuweka jiji safi wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa 'Dustbin'
53 zilizotolewa na Burhani Foundation Tanzania iliyofanyika katika
mskiti wa dhehebu la Mabohra nchini.
Kiongozi
Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal
bhaisaheb Saifuddin moja ya Dustbin kati ya 53 zilizotolewa na Burhan
Foundation kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi katika hafla fupi
iliyofanyika nyumbani kwa Kiongozi huyo jijini Dar es Salaam.
Kiongozi
Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal
bhaisaheb Saifuddin akimvisha kikoi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi na kumwombea dua baada ya kukabidhi Dustbin 53 kwa ajili ya
manispaa ya Ilala.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akimshukuru Kiongozi Mkuu wa dhehebu
la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin
kwa zawadi ya kikoi.
Afisa
Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda
akipokea zawadi ya kikoi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi
Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin.
Mwenyekiti
wa CCM, Serikali za Mitaa Kata ya Kisutu, Mustaquim Darugar (kushoto)
akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Ikiwa
ni wiki ya mazingira duniani, Wilaya ya Ilala imeeleza mipango yake ya
kuweka mazingira katika hali ya usafi kusambaza makasha yatakayotumika
kuhifadhia taka baada ya kupokea msaada wa makasha 53 kutoka Taasisi ya
Burhani.
Akipokea
msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi alisema wilaya yake
imeanza kujipanga katika hilo ili kuweka mazingira safi na kuwataka
wananchi wote kutupa taka katika makasha hayo mara tu baada ya kumaliza
matumizi yao.
Alisema
jukumu la kuweka mazingira katika hali ya usafi nila kila mmoja hivyo
kila mtu ana wajibu wa kushiriki kuweka mazingira yanayomzunguka katika
hali ya usafi jambo ambalo linaweza kusaidia kuondokana na magonjwa ya
mlipuko ambayo mara nyingi yamekuwa yakisababishwa na uchafu uliosambaa
katika mazingira yanayotuzunguka.
“Kwa
wananchi wote hata kama ukinywa maji au kula embe, ndizi na hata kama ni
vocha au umetumia sigara uchafu wote uwekwe katika makasha hayo ili
tuweze kuweka wilaya katika usafi na uchafu huo utakuwa unakuja
kuchukuliwa na watu ambao tumewaweka kufanya kazi hiyo,
Afisa
Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda
(kulia) akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati)
kuzindua wiki ya mazingira duniani pamoja na kuzungumza na wakazi wa
mtaa wa Sea-View pamoja na wafanyakazi wa makampuni ya usafi ikiwemo
Geen Waste Pro Ltd. Kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
Sea-View Upanga, Victor Muneni.
“Wilaya
yetu imejipanga kwa sasa kusambaza makasha katika mazingira yetu na
katika kata zote ni wajibu wa kila mmoja kushiriki kuweka mazingira
katika hali ya usafi uchafu wote unatoka katika mazingira yetu hatuna
budi kushirikiana kufanya usafi,” alisema Raymond.
Kwa
upande wa Taasisi ya Burhani ambao ndiyo wametoa msaada kupitia
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohra, Muslim Hassuji alisema wametoa msaada
huo ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Magufuli kuweka mazingira
katika kusaidia kuweka mazingira safi na pamoja na msaada huo pia
wamejipanga kuendelea kutoa msaada wa vifaa katika maeneo mengine ya
jiji la Dar es Salaam.
“Tunamuunga
mkono Rais wetu Magufuli ili tuweke mazingira yetu safi, msaada huu wa
makasha ya kuhifadhia taka 53 kwa wilaya ya 53 ni awamu yetu ya kwanza
na tutaangalia jinsi yatakavyofanya kazi na baada ya hapo tutatoa
mengine na baadae tugawe hata kwa mkoa wote wa Dar es Salaam,” alisema
Hassuji.
Nae
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafi ya Green West Pro Limited, Anthony Mark
aliwataka Watanzania wabadilike na kuwa na kujiwekea utaratibu kuweka
mazingira yanayowazunguka safi kutokana na wengi wao kujisahau kufanya
usafi.
“Watanzania
wengi sio wastarabu unakuta mtu yupo ndani ya gari anakunywa hata maji
akimaliza anatupa kopo nje hii sio tabia njema inatakiwa ifike hatua
tubadilike na tushiriki kuweka mazingira yetu safi sio wengine wanafanya
wengine hawashiriki,” alisema Mark.
Aidha
Mkurugenzi huyo wa Green West Pro aliwatupia lawama Shirika la Umeme
nchini (TANESCO) kwa tabia ya kuacha miti ambayo wamekuwa wakikata kwa
madai ya kuwa karibu na nguzo za umeme na baadae kuiacha.
Alisema
sio ustaarabu kwani kufanya hivyo ni kuchafua mazingira na kuwaachia
wananchi uchafu ambao haukusababishwa na wao na hivyo kuwataka
kubadilika ili kusaidia kuweka mazingira safi kama jinsi Rais Magufuli
anavyoagiza.
Nae
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Bw. Abdon Mapunda alisema kuelekea kilele cha wiki ya mazingira
wataendelea kushiriki katika maeneo mbalimbali kufanya usafi ikiwa ni
kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ambapo kwa kuanza hapo
jana Jumatano walishirikiana na Kampuni ya Usafi ya Green West Pro ltd
ambapo walifanya usafi katika eneo la Salender Bridge.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akitoa maagizo kwa Kamanda wa kituo
cha Polisi Salender Bridge kuhusiana usafi wa mazingira kuzunguka maeneo
yao katika fukwe za bahari ya Salender.
Mkaazi
wa mtaa wa Sea-View mzee Peter Kabelwa almaarufu kama Mzee Mzungu
akishiriki zoezi la kuondoa uchafu uliozunguka katika fukwa za bahari ya
Salender Bridge.
Mwanamazingira kutoka Roots and Shoots akishiriki kukusanya taka zilizosambaa kwenye eneo la fukwe za bahari ya Salender Bridge.
Mkurugenzi
wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Anthony Mark Shayo na
Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Abdallah Mbena (kulia) wakishirikiana
na wafanyakazi wa kamouni hiyo kufanya usafi kwenye eneo la fukwe za
bahari ya Salender Bridge.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na wadau wa mazingira wakiendelea na zoezi la usafi kwenye fukwe hizo.
Afisa
Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda
(katikati) akishiriki zoezi la usafi kwenye fukwe za bahari ya Salender
Bridge.
Eneo hili lilisahaulika kwa muda mrefu bila kufanyiwa usafi kitu ambacho ni hatari kwa samaki wanaoishi kwenye fukwe hizo.
Muonekano wa fukwe za bahari ya Salender Bridge kabla ya kusafishwa na wadau wa mazingira wakiwemo Green Waste Pro Ltd.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akiagana na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Usafi ya Green West Pro Limited, Anthony Mark baada ya kuzindua wiki ya
mazingira Manispaa ya Ilala ambapo dunia kote inaadhimisha.
No comments:
Post a Comment