Mkurugenzi
Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha (wa pili kulia),
akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla
waliyowaandalia wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika
kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara.
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka
kushoto ni, John Kazimoto, Jones Mwalemba, naJohn Du Toit.
Mkurugenzi
Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha ( kulia), akizungumza na
baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia wateja wao
kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma
bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika
jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka kushoto ni, John
Kazimoto na Jones Mwalemba.
Mkuu
wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk.
Mabouba Diagne (wa pili kulia), akibadikishana mawazo na baadhi ya
wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia wateja wao
kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma
bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika
jijini Dar es Salaam juzi.
Mkuu
wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk.
Mabouba Diagne (wa pili kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki
hiyo, John Du Toit katika hafla waliyowaandalia wateja wao kuwajulisha
mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki
chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam
juzi.
Mkuu
wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni BancABC Tanzania,
Khalifa Zidadu (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo
katika hafla waliyowaandalia wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki
hiyo katika kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la
atlasmara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni
Ofisa Fedha Mkuu wa Superdoll, Sateesh Babu Desu na Prasanthar Govinder
pia wa Superdoll.
Mkurugenzi
Mtendaji wa BancABC Tanzania Bwana. Dana Botha ( kulia), akizungumza na
baadhi ya wateja wa benki hiyo (hawapo pichani) katika hafla
waliyowaandalia wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika
kuhakikisha wanatoa huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara.
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wanaomsikiliza kutoka
kushoto ni, John Kazimoto na Jones Mwalemba.
Mkuu
wa Idara ya Uwekezaji wa Kibenki ya Makampuni wa Kundi la BancABC, Dk.
Mabouba Diagne (wa pili kulia), akifafanua jambo mbele ya baadhi ya
wateja wa benki hiyo (hawapo pichani), katika hafla waliyowaandalia
wateja wao kuwajulisha mikakati ya benki hiyo katika kuhakikisha wanatoa
huduma bora za kibenki chini ya kundi la atlasmara. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Bank
ABC imeanzisha huduma mpya kwa wafanyabishara wakubwa kuhamisha and
kuingiza mitaji yao ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia ya
kisasa ya elektroniki.Akizungumza katika hafla iliyofanyika Jumatano
hii, Mkuu wa kundi la Benki hiyo katika ukanda wa Afrika, Dk. Mabouba
Diagne alisema wametenga Dola za Kimarekani milioni 20 (zaidi ya Sh
billion 40) kwa ajili ya mpango huo unaolenga kuimarisha biashara
miungoni mwa nchi za Afrika.
“Tumeanzisha
huduma hii mpya kwa ajili ya kurahisisha na kukuza biashara miungoni
mwa wafanyabishara wakubwa barani Afrika. Tunataka wafanyabiashara
waweze kufungua milango yenye fursa nyingi za kibishara barani Afrika,”
Dk. Diagne alisema.Alisema Banc ABC imezimia kuwawezesha Watanzania
kutumia teknolojia mpya ya kuhamisha mitaji na fedha nyingi si ndani ya
nchi tu bali nje ambako kuna fursa nyingi za biashara zisizotumika.
“Mara
nyingi wafanyabishara wengi wa hapa nchini wanaofanyabishara nan chi
jirani wamekuwa wakilalamika kukosekana kwa huduma bora za kuhamisha
fedha kwa wingi. Sasa jawabu limepatikana kwa Banc ABC kuanzisha huduma
za kisasa za kuhamisha mitaji,” alisema.
Alisema
watu wanaweza kuhamisha mitaji hata fedha nyingi nchi za nje kwa
kutumia simu za mkononi bila kuathiri biashara.“Tumeanzisha huduma hii
kwa sababu biashara baina ya nchi za Afrika ni jambo muhimu la kuwezesha
nchi na wafanyabishara waweze kutumia fursa nyingi zilizomo barani
Afrika kutokana na bara hili kuwa na rasilimali nyingi asilia,” alisema
kiongozi huyo msomi mwenye shahada ya juu ya uzamili ya hisabati.
Alisema
suala la kubadilishana na kuhamisha mitaji ni biashara kubwa duniani
kwa sababu mitaji ni bidhaa muhimu kwa maendeleo ya nchi na watu.Mapema
mkurugenzi wa Banc ABC Tanzania, Bw Dana Botha alisema tayari benki hiyo
imeanzisha mtandao wa matawi 100 hapa nchini na kuwa miungoni mwa benki
imara.Naye Mtendaji Mkuu wa kundi la benki hiyo Dk. Blessings Mudavanhu
alisema kuwa benki hiyo ambayo imesajiliwa katika soko la fedha la
London, ilizindua aina ya bidhaa yake mpya na kujitanua kimataifa baada
ya kuungana na Atlas Mara.
“Tutatumia
jamvia la teknolojia ya habari na mawasiliano. Tunataka watu waanchane
na kuandika cheki nyingi na kutumia gharama kubwa za miamala ya katatazi
badala yake watumie simu za mkononi,” alisema Dk Madavanhu.Alisema
benki hiyo ambayo inaendesha biashara katika nchi za Tanzania, Nigeria,
Afrika kusini, Botswana Zimbabwe, Rwanda, Burundi na Zambia imedhamiria
kuwa benk kubwa inayokuza biashara miungoni mwa nchi za Afrika.
Katika
hafla hiyo kampuni kadhaa kubwa zilishiriki na kuvutiwa na huduma hiyo
mpya itakayotolewa na benki hiyo ya kimataifa. Kampuni hizo ni; Statoil,
Mount Meru (T) Ltd, Lake Oil. Superdoll na Puma Energy.
No comments:
Post a Comment