Usiku wa June 13 2016 jina la Rais wa zamani wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Sepp Blatter
lilirudi kwenye headlines, baada ya Rais huyo kutoa kauli ambayo
inaeleza udanganyifu ambao unafanyika katika michuano ya Ulaya.
Blatter ameeleza kuwa kuna baadhi ya mashinda yanayoandaliwa na UEFA
huwa yanafanya udanganyifu katika uchezeshaji wa droo za makundi ya
michuano hiyo, licha ya kutotaja michuano iliyiwahi kufanya
udanganyifu huo, Blatter alieleza kuwa vipira vinavyowekwa katika chungu utofautishwa kwa vingine kuwa vya moto na baridi.
Katika udanganyifu huo Blatter ameeleza kuwa kuna timu moja tu ndio haijawahi kunufaika na uongo huo, kama utakuwa unakumbuka vizuri Blatter aliwa Rais wa FIFA toka mwaka 1988 na alijiuzulu wadhifa huo 2015, baada ya kutuhumiwa kuhusika katika makosa kadhaa ikiwemo rushwa.
No comments:
Post a Comment