Pages

June 6, 2016

MWIGULU NCHEMBA APOKELEWA KWA SHANGWE JIMBONI KWAKE IRAMBA

Waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akifurahia zawadi ya maboga aliyepewa na wananchi wa kijiji cha KilaMpanda jimbo la Iramba mkoa wa Singida wakati wa ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kumchagua bila kufanya kampeni mwaka jana kuendelea kuwa mbunge wao kwa kipindi cha pili sasa.
Wananchi wa jimbo la Iramba kata ya Kilampanda wakimpokea mbunge wao Bw Mwigulu Nchemba kwa zawadi za maboga wakati wa ziara yake jimboni humu jana Juni 5.
Mbunge wa jimbo la Iramba ambae ni waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akikabidhiwa zawadi ya boga na wananchi wa kijiji cha Kilampanda wilaya ya Iramba mkoa wa Singida wakati wa ziara yake jimboni humo Juni 5 kwa ajili ya kuwashukuru na kutekeleza ahadi zake.
Mbunge Nchemba akiteta jambo na katibu wake Bw Daud Ntukuna kushoto
Wananchi wa kata ya Kilampanda wakimpokea mbunge wao Bw Nchemba kwa matawi ya miti.
Mwigulu Nchemba akipokelewa kwa shangwe jimboni kwake Iramba
Mbunge Nchemba akiwapungia mikono wananchi wake baada ya kupokelewa wakati wa ziara ya kuwashukuru kwa kumchagua.
Mmoja kati ya wananchi akimshukuru mbunge Nchemba kushoto kwa utekelezaji wa ahadi zake jimboni
Mbunge Nchemba akimpa mpiga kura wake namba yake ya simu
Mbunge Nchemba akiwasili kijiji cha Kilampanda kwa ziara.
mwananchi wa kata ya kilampanda akimkumbatia mbunge Nchemba kwa furaha.
Mbunge wa Iramba na waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi akipokelewa jimboni kwake.
katibu wa CCM Iramba akimkaribisha mbunge Mwigulu
Mbunge wa jimbo la Iramba na waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi akikabidhi ahadi yake ya bati kwa wananchi wa kijiji cha Kilampanda kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afaya hadi sasa amegawa bati 1800 zenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 45 kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa wananchi hao kwa lengo la ujenzi wa Zahanati ,mabweni , vyumba vya madarasa na nyumba za walimu na waganga ,nondo 450 zenye thamani ya zaidi tsh milioni 7.6
Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba akifurahia zawadi ya mbuzi aliyopewa na wananchi wake wakati wa ziara ya kuwashukuru kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu mwaka jana pasipo kufika kufanya kampeni ,Mwigulu amekuwa akitumia siku za mapumziko bungeni kuzunguka jimboni mwake kufanya mikutano ya kushukuru wananchi kila Jumamosi na jumapili.
Mbunge Mwigulu akitembea kwa miguu na wananchi wake katika moja kata ya bonde ambalo ni hesemu ya barabara inayolalamikiwa na uwananchi kutokana na ubovu eneo hilo halina daraja.
gari la waziri likipita eneo korofi la barabara.
waziri Nchemba akiwa na wapiga kura wake.
Lori lililobeba bati ambalo husambaza ahadi za mbunge Mwigulu jimboni.
Mbunge Mwigulu akisalimiana na wapiga kura wake.
Mbunge wa jimbo la Iramba Bw Mwigulu Nchemba akiongea na vijana kwa ajili ya kuwasaidia vifaa vya michezo wakati wa ziara yake jimboni humo jana juni 5. PICHA NA MATUKIODIMABLOG.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...