Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimuapisha Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika
hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Pichani Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein
akiwa katika picha na Said Hassan Said Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
na familia yake baada ya kumuapisha rasmi leo katika hafla iliyofanyika
Ikulu Mjini Zanzibar.
Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said akipitia hati ya kiapo kabla ya
kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.ALi Mohamed Shein hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini
Unguja.
Mkurugenzi
wa Mashtaka Zanzibar Nd,Ibrahim na Mzee na Mrajis wa Mahkama Kuu
Zanzibar George Kazi ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla
ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said leo Ikulu
Mjini Unguja.
Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Abdalla Mwinyi Khamis na Mstahiki Meya wa
Zanzibar Khatib Abrahman Khatib ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria
katika hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said
leo Ikulu Mjini Unguja.
Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said akiwa katika ukumbi wa mikutamo Ikulu
Mjini Unguja na Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mshibe Ali Bakari
kabla ya kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein.
Viongozi
mbali mbali na watendaji waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Said
Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika ukumbi wa mikutano
Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment