Mmoja
wa Mashabiki wa Tamasha la Pasaka pamoja na mashabiki wengine
waliohudhuria katika Tamasha la Pasaka lililofanyika mjini Geita Mkoani
Geita kwenye ukumbi wa Desire wakiimba kwa kuzinguka ukumbi huo wakati
mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani na
kuwafanya wavutiwe na tamasha hilo kiasi cha kushindwa kukaa kwenye viti
wakizunguka huku na kule huku baadhi wakiwa wabebeba viti juu juu.
Katika
Tamasha hilo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie
akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili waliohudhuria katika
tamasha hilo ameishukuru kampuni ya Msama Promotion na Mkurugenzi wake
Bw. Alex Msama kwa kuandaa tamasha hilo kwani hiyo ni fursa pekee ya
baadhi ya wananchi wa mkoa wa Geita kumrudia Mungu na kutubu ili kuacha
tabia mbaya inayoupaka matope mkoa huo kwa mauaji ya walemavu wa ngozi
Albino pamoja na Vikongwe
Waimbaji
mbalimbali wameshiriki katika tamasha hilo ambao ni Upendo Nkone, Bonny
Mwaiteje, Joshua Mlelwa, Martha Baraka, Jesca BM, Jennifer Mgendi,
Mwimbaji kutoka Zambia Ephraim Sekereti, Waimbaji kutoka Nchini Kenya
Solomon Mukubwa , na Mtanzania Faustine Munishi pamoja naye Christopher
Muhangila.
Matamasha
hayo yataendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na
keshokutwa litafanyika tamasha lingine kama hilo mjini Kahama mkoani
Shinyanga.
Tamasha
la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion chini ya
mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa udhamini wa magazeti ya Dira, Dira
TV na Dira FM na linafanyika kila mwaka katika kipindi cha sikukuu za
Pasaka (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-GEITA)
Mwimbaji Jesca BM akifanya vitu vyake jukwaani.
Mashabiki wake wakiitikia na kuimba kwa hisia wakati mmwibaji huo akiimba jukwaani.
Mkurugenzi
wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akirekebisha sauti katika mitambo
wakati tamasha hilo likiendelea huku DJ akiangalia.
Mama akifurahia uimbaji na uponyaji kutoka kwa waimbaji katika tamasha hilo huku akiwa amemshikilia mtoto wake mchanga.
Maadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakifuatilia waimbaji kwa makini.
Mwimbaji Martha Baraka na kundi lake wakitumbuiza jukwaani huku baadhi yamashabiki wakipata picha kwa simu.
Mwimbaji Jennifer Mgendi naye akafanya mambo makubwa jukwaani kama anavyoonekana.
Mwimbaji
Ephraim Sekereti akisalimiana na mdau mkubwa wa Msama Promotion Bw.
Silas huku akitaniana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie wa
tatu kutoka kushoto waliosimama mara baada ya kumaliza kuimba.
Mwimbaji
Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba jukwaani huku mgeni rasmi
Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akicheza pamoja na Mkurugenzi
wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na mashabiki wengine.
Mwimbaji Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake walioonekana kuhamasika na nyimbo zake.
Mwimbaji Bonny Mwaiteje naye akafanya mambo makubwa jukwaani huku akipewa sapoti na mashabiki wake.
Mwimbaji
Bonny Mwaitege akiwa amewabeba wacheza shoo wake mara baada ya kumaliza
kuimba jukwaani hii ilikuwa ni staili ya aina yake.
mgeni
rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akitoa salamu zake za
shukurani kwa kampuni ya Msama Promotion kwa kuandaa tamasha la pasaka
katika mkoa wa Geita wilaya ya Geita kwa ni jambo jema kuwahubiria amani
wananchi wa Geita ili wamrudie Mungu na kuacha mauaji ya Albino na
Vikongwe.
Waimbaji
Solomon Mukubwa kulia , Bonny Mwaiteje kushoto wakimpiga tafu Mwimbaji
mwenzao Christopher Muhangila katikati wakati alipokuwa akitumbuiza
jukwaani.
No comments:
Post a Comment