Baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi hicho wakiendelea na majumu yao.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee,
Dkt. Hamisi Kigwangalla amekutana kwa mara ya pili na kikosi kazi cha
watu 24 ambacho kitakuwa na kazi ya kutengeneza mpango mkakati wa
kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Mkutano
unaoendelea katika ukumbi wa Wizara hiyo ya Afya, leo Februari 20th,
2016 unachambua mambo mbalimbali ya kuweza kuyafanyia maboresho na ya
kimkakati ilikuweza kufikia malengo ya Mfuko huo wa Afya ya Jamii (CHF).
Katika
Mkutano huo, Dkt. Kigwangalla ni mwenyekiti wa kikosi kazi hicho
ambapo kwa ujumla na wajumbe hao wapo kupanga mikakati thabiti.
Baadhi
ya Wajumbe wa kikosi kazi hicho wanaoshiriki kikao ni pamoja na Prof.
Angwara Kiwara, Prof. Phares Mujinja, Dkt. Francis Frederick, Dkt. Heri
Marwa, Dkt. Deogratius Pisa, Dkt. Amos Kahwa, Irene Kiria, Semkae
Kilonzo, Gemini Mtei, Dkt. Jehovaness Aikaeli na Obey Assey.
Wengine
ni Mathias Kabunduguru, Dkt. Dereck Chitama, Prof. Flora Kessy,
Florence Mwanri, Athuman Rehani, Maximillian Mapunda, Bedason Shallanda,
Daniel Ngowi, Beng' Issa, Edwin Mikongoti, Hussein Sengu, Dkt. Beatus
Leon na Dkt. Pastory Sekule.
imeandaliwa na Andrew Chale,modewjiblog
Mkutano huo ukiendelea.
Baadhi
ya wajumbe wa kikosi kazi hicho wakimsikiliza Naibu Waaziri wa Afya
Dkt.Kigwangalla (Hayupo pichani) wakati wa mkutano huo unaoendelea
Wizarani hapo.
Naibu
Waziri Dkt.Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho
(kulia) akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe hao. (Picha zote na Andrew
Chale,modewjiblog).
No comments:
Post a Comment