Pages

December 14, 2015

Kauli za wachezaji 6 wa zamani wa Man United wanaoamini Louis van Gaal anaibomoa Man United …

Headlines za mfumo wa kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal katika kukifundisha kikosi hicho zinazidi kuchukua nafasi kila siku. Tumewahi kuwasikia wachambuzi kadhaa wa soka ambao wamekuwa wakitaja kuwa uwezo na mbimu za kocha huyo sio nzuri kitu ambacho kinapelekea Man United kutofanya vizuri.
December 14 naomba nikusogezee kauli za wachezaji sita wa zamani wa Man Unitedwanaoamini kuwa Louis van Gaal anabomoa mfumo wa uchezaji wa Man United.
6- Roy Keane
Roy Keane of Manchester Utd and Arsenal's Patrick Vieira come to blows during the game at Arsenal's  Highbury ground, Sunday August 22, 1999. Final score 1-2 to Man Utd. Photo by Sean Dempsey/PA
“Ana kikosi chenye wachezaji wazuri haitaji kutafuta wengine nje ya kikosi, angalia wakati alipoingia Man United wametupa fedha nyingi kusajili ila bado hana wachezaji maalum hadi sasa” >>> Roy Keane
5-Peter Schmeichel
Schmeichel1
“Kihistoria mashabiki wa Man United wanahitaji kitu cha ziada, Man United walikuwa wanacheza soka la kuburudisha, mchezo ambao uliletwa na  Alex Ferguson. Hiki ndicho kinacholalamikiwa na mashabiki wa Man United kwani wanahitaji soka la kuvutia” >>> Peter Schmeichel
4- Rio Ferdinand
Rio-EPL
“Zamani Man United ilikuwa ni kawaida kuona katika timu tatu au nne za juu kuna wachezaji ambao ni viongozi, unaposema umetumia pound milioni 250 kufanya usajili na kusema kuwa umefunga usajili, baada ya hapo unasema Man United haiwezi kushindana katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya, hii inashangaza” >>> Rio Ferdinand
3- Michael Owen
Owen-United
“Nafikiri licha ya kutumia fedha zote hizo katika usajili nafikiri ana kikosi kibovu kuliko kilichokuwa awali, Louis van Gaal katika kipindi cha miezi 18 tu kaacha wachezaji kadhaa waondoke Man United. Tulikuwa na wachezaji wazuri kama Vidic, Evra, Nani, Kagawa, Cleverley, Robin van Persie na Chicharito” >>> Michael Owen
2- Garry Neville
Roy Keane of Manchester Utd and Arsenal's Patrick Vieira come to blows during the game at Arsenal's  Highbury ground, Sunday August 22, 1999. Final score 1-2 to Man Utd. Photo by Sean Dempsey/PA
“Van Gaal hakutakiwa kukurupuka kuwajibu waandishi wa habari kuwa sisi hatujui kitu kwani kufanya hivyo ni kuwaambia mashabiki, mashabiki wanafikiria kama alichokiandika Neville, ukweli ni vigumu sana kuangalia dalili za hatari” >>> Garry Neville
1- Paul Scholes
Scholes-United
“Kiukweli kikosi anakifundisha kujihami zaidi kuiko kucheza soka la kushambulia kufunga magoli na kuweka ubunifu. Kwa sasa Man United ni timu ambayo hutopenda kucheza dhidi yake au kucheza ndani ya kikosi hicho ” >>> Paul Scholes

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...