Pages

May 1, 2015

WAFANYAKAZI WAHIMIZWA KUJITOKEA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura ili kuweza kupiga kura ya maoni na kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
Hayo yamedhihirika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei 1, 2015 zilizofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wizara mbali mbali ikiwemo taasisi binafsi zilibeba mabango yenye ujumbe kuhamasisha wafanyakazi.
Mpaka sasa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linaendelea vizuri katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
 Wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) wakiwa katika maandamano kusherekea siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI huku wakiwa na bango lenye ujumbe wao mahususi kuwahamasisha wananchi kushiriki kujiandikisha na wapige kura kuchagua kiongozi bora.
 Wafanyakazi wa Mamlaka  ya anga nao  hawakuwa nyuma na mabango yao.
 Wafanyakazi wa Ofsi ya Rais - Ikulu...
 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege ya Air Tanzania...
Mabango mbalimbali yamebeba kaulimbiu juu ya kuhamasisha wafanyakazi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura km.(Picha na Christina Njovu).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...