Pages

May 1, 2015

MEYA AMIRI NONDO ANOGESHA KONGAMANO LA WAANDISHI WA HABARI KUELEKEA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MEI 2/ 2015 MORO.


Mweka Hazina wa Morogoro Press Club kushoto, Lilian Lucas, Mwenyekiti mstaafu wa Club hiyo, Azizi Msuya, Frank Odomare na Fitina Haule wakimsikiliza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano la uhuru wa vyombo vya habari Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG

 
Kongamano hilo limeenda sambamba na maandalizi ya kuwanoa waandishi wa habari ambao watakuwa wenyeji wa maadhimisho ya kilele cha siku ya uhuru wa vyombo vya habari itayoadhimishwa kitaifa mkoani Morogoro Mei 02/2015, Nashera Hoteli mkoani hapa ikiwaimebeba kauli mbio "uandishi bora, zama za kidigitali".
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo akifungua semina huku Katibu wa Morogoro Press Club, Abeid Ramadhani Dogoli na Mlezi wa klabu ya waandishi wa habari Morogoro (MoroPC) Steven Mashishanga wakifuatilia jambo katika kongamano hilo.

Makamu Mwenyekiti wa Morogoro Press Club, Nickson Mkilanya akizungumza jambo katika kongamano hilo, kulia ni Meya Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo na kushoto ni Mratibu wa Morogoro Press Club Thadei Hafigwa na Rashid Lusewe ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya club hiyo.
Frank Odomari, Fitina Haule Ashura Kazinja wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa kongamano hilo wakati Meya wa Manispaa ya Morogoro akizungumza jambo katika ukumbi wa jengo la golofa la walimu mtaa wa Nunge.
Vijana wa Mwananchi McNamara Ngambi kulia na Peter Kimath wa JamboLeo wakibadilishana mawazo.
Mwandishi wa Clouds FM mkoa wa Morogoro, Merina Robert akimweleza jambo Meya wa Manispaa (hayupo pichani).
Mwandishi mkongwe wa gazeti la Majira mkoa wa Morogoro, Halfan Diyu akichangia kwa kutoa hoja kwa Meya wa Manispaa hiyo, Amiri Nondo.
Mlezi wa klabu ya waandishi wa habari Morogoro (MoroPC) Steven Mashishanga akizungumza jambo katika kongamano. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Nickson Mkilanya na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo.
MSTAHIKI MEYA wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Juma Nondo wa pili kutoka kushoto waliokaa mtastaa wa mbele, Mwenyekiti wa Moropc Idda Mushi, Mwenyekiti wa maadili club hiyo, Rashid Lusewa na Mlazi wao, Steven Mashishnga wa kwanza kushoto katika mstari huo wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari na viongozi wengine waandamizi wa klabu ya waandishi wa habari Morogoro mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo leo lililofanyika jengo la walimu Nunge.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...