Pages

May 7, 2015

MESSI, NEYMAR WAIUA BAYERN, BARCELONA IKISHINDA 3-0

Na Richard Bakana
Washambuliaji wa Timu za Taifa za Argentina, Lionel Messi pamoja na Brazil, Neymar JR usiku huu wasaidia klabu ya ya Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya.
Baada ya dakika 45 za kwanza kukata timu zote zikiwa hazijafungana licha ya kutengeneza nafasi kadhaa ambazo timu zote zilishindwa kuzitendea haki, Messi 10 alianza kufungua ukurasa wa mabao kunako dakika ya 77 baada ya kuachia shuti kali kwa mguu wa ushoto na lililomshinda mlinda mlango wa Bayern, Manuel Neuer.
Haikuchukua muda mrefu kwa kunako dakika ya 80 Messi kwa mara nyingine akipenyezewa pasi safi na Iniesta ambapo alimtpiga chenga Boateng hadi kukaa chini na kukutana na Manuel Neuer ambaye alipishana na mpira ukiingia langoni baada ya Messi kuuchop na kutinga langoni.
Katika dakika ya 90 Neymar JR akafunga kitabu cha mabao kwa kuandika goli la tatu na kufanya matokeo yawe 3-0.

VIKOSI VILIVYOCHEZA NI KAMA IFUATAVYO
Barcelona: Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano, Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta, Suárez, Messi, Neymar
Subs: Bravo, Xavi, Pedro, Rafinha, Bartra, Adriano, Vermaelen
Bayern Munich: Neuer, Rafinha, Benatia, Boateng, Lahm, Alonso, Thiago, Bernat, Schweinsteiger, Müller, Lewandowski
Subs: Reina, Dante, Martinez, Pizarro, Gaudino, Götze, Weiser

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...