Mchezo wa ngumi ni mmoja ya michezo maarufu na inayopendwa zaidi duniani.
Pambano la May 2 2015 kati ya Floyd Mayweather na mpinzani wake Manny Pacquiao lilidhihirisha kwamba kumbe kuna mashabiki wengi duniani wanaopenda mchezo wa ngumi.
Forbes imetoa orodha ya mabondia ambao wanaongoza kwa utajiri mkubwa zaidi duniani;
No.1- Floyd ‘Money’ Mayweather: Mbabe huyu ndio tajiri zaidi kwa mabondia duniani.. Utajiri wake ni kama dola Mil. 380.
No.2: George Foreman: Anashika
nafasi ya pili kwa utajiri kwa utajiri wa dola Mil. 250, alistaafu
ngumi za kulipwa kwa sasa ni mjasiriamali na mwigizaji.
No.3- Oscar De La Hoya:
Utajiri wake ni dola Mil. 175, mpaka anastaafu mwaka 2009 alikuwa na
ushindi wa mapambano 39 kati ya 45 aliyowahi kucheza. Huyu ni raia wa
Mexico.
No.4- Lenox Lewis: Jamaa
ana uraia wa Uingereza na Canada.. Utajiri wake ni kama dola Mil. 140
hivi, aliingia kwenye headlines baada ya kuwapiga mabondia kama Mike Tyson mwaka 2002.
No.5: Emmanuel ‘Manny’ Dapidran Pacquiao: Raia wa Ufilipino ambae aliingia kwenye headlines baada ya kupigwa na bondia Mayweather
May 2 2015 Marekani.. Bado yuko vizuri kwenye nafasi ya tano na utajiri
wake wa dola Mil.120.. mapato yake yanatokana na mchezo wa Ngumi,
matangazo ya biashara, pamoja na posho za Ubunge nyumbani kwao
Ufilipino.
No.6- Sugar Ray Leonard:
Ni bondia Mmarekani aliyestaafu akiwa na record kubwa pia, katika
mapambano yake 40 alishinda jumla ya mapambano 36. Baada ya kustaafu
mwaka 1997 aliamua kujishughulisha na uchambuzi wa Michezo pamoja na
kucheza movies.
No.7- Vitali Klitschko:
Utajiri wake ni kama dola milioni 65. Jamaa baada ya kustaafu boxing
akaamua kuingia kwenye siasa, kwa sasa ni Meya wa Jiji la Kiev, nyumbani
kwao Ukraine.
No.8- Muhammad Ali:
YES.. Dunia inatambua record ya huyu bondia, kwa sasa anajishughulisha na
masuala ya Harakati za Mambo ya Kijamii Marekani.. Utajiri wake ni dola
Mil. 50. Moja ya aka alizowahi kupewa ni The Greatest.
No.9- Marvin Hagler:
Ni bondia wa Marekani ambaye alistaafu akiwa na record ya kushinda
mapambano 62 kati ya 67 aliyowahi kucheza. Baadae akaingia kwenye ishu
ya kucheza movie.. Utajiri wake ni dola Mil. 45
No.10- Bernard Hopkins: Jamaa aka yake anaitwa The Executioner, ni bondia ambaye anapigana ngumi za ubingwa wa dunia kwa uzito wa kati, ana utajiri wa dola Mil. 40
Chanzo.MilladAyo
No comments:
Post a Comment