Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya kompyuta
maalum zinazotumiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi
mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na
Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu,
kompyuta, magari na darubini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijaribu akikagua moja ya vitanda na hema linazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akishuka kutoka basi linalotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikwagua gwaride la heshima
jana alipowasili Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza
alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya
Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari
na darubini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijaribu moja ya darubini zinazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia vifaa vinavyotumiw ana wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi
mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na
Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu,
kompyuta, magari na darubini.
Picha ya pamoja ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza.
Serikali
imesema kwamba itaanza kuwaajiri moja kwa moja askari wa wanyamapori
kama inavyofanyika kwa jeshi la polisi na Jeshi la wananchi Tanzania
(JWTZ).
Akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Wanyamapori cha Pasiansi jijini Mwanza jana Waziri a Maliasili
na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema utaratibu unaotumika kw asasa
unaleta usumbufu kwani urasimu unasababisha askari hao wanapomaliza
mafunzo kusubiri kusailiwa wakati wa ajira wakati kuna upungufu mkubwa
wa askari hao.
“Hatuwezi
kukaa na kusubiri kupata kibali cha sekritarieti ya ajira kwa maana
sasa hivi tumeanzisha Mamlaka ya Wanayamapori na kwa hiyo watakuwa na
uwezo wa kuajiri mojakwa moja kuliko utaratibu wa sasa unaofanya
mwanafunzi akimaliza chuo asubiri kusailiwa mbona polisi na jeshi
hawafanyi hivyo?”
Waziri
Nyalandu alisema kwa sasa kuna tatizookubwa kla ujangili na kuahidi
kuwa vijana wengi watakaopata mafunzo wataajiriwa ili vita ya kupambana
na majangili nchini ielekezwe sehemu zote ili kuweza kulinda na
kuhifadhi rasilimali nchini kwa ajili ya vizazi vijavyo.
“Tumefanikiwa
Serengeti na Selous lakini kwa sasa janga kubwa limekuwa katika pori la
Rungwa ambalo limeungana na Ruaha, Tembo wengi wamekuwa wakiuawa na
sasa vita tunaelekeza huko, ili kumaliza tatizo la ujangili”.
Alisema
kuwa majangili watatafutwa popote wqlipo na kwamba wananchi wanatakiwa
kuingia katika vita hiyo na kutoa taarifa zitakazosababisha majangili
kukamatwa sehemu yoyote walipo ikiwa ni pamoja na ndugu zao na wafadhili
wao.
Nyalandu
ambaye alitembelea chuo hicho kukagua maendeleo ya mradi wa maboresho
ya chuo unaofadhiliwa na Howard Buffet Foundation (HGBF) kwa kupitia
taasisi yake ya uhifadhi ya Nature Conservation Trust aliagiza ujenzi wa
bweni la wanafunzi 300 ukamilike katika kipindi kifupi kwa kuwa pesa za
mradi zipo tayari.
Mkuu
wa chuo hicho, Lowaeli Damalu alimshukuru Waziri Nyalandu kwa kutafuta
mfadhili huyo na kusema kuwa kwa sasa chuo kimekuwa ch kisasa na vifaa
vya kutosha kw akufundishia.
Alisema
kwamba msaada huo unaokaribia Sh4bilioni umewezesha kununua vitabu
magari, mahema darubini na kompyupa ambavyo unaweza kuwajenga wanafunzi
kufanya kazi watakapoajiriwa kwa weredi mkubwa.
Dumalu
alisema kwamba kwa sasa bwalo la chakula limekamilika na fedha kwa
jaili ya ujenzi wa bweni ziko tayari lakini tatizo limekuwa ni kwa
mkandarasi ambaye aliweka bei kubwa kupita bajeti na hivyo kumwahidi
waziri kuwa mkandarasi ataletwa na mfadhili ili kukamilisha mradi huo
kabla ya mwisho wa mwaka.
Alisema
mbali na kuboresha mafunzo kwa wanafunzi lakini pia walimu wamepata
fedha kutoka HGBF kwa ajili ya mafunzo kwa walimu na wafanyakazi ambao
wamekuwa wakiendelea na mafunzo hayo kazini ili kuweza kupambana na
ujangili na kwamba mradi huo bado unaendelea na kuwa mfadhili huyo
tajiri namba mbili Marekani yuko tayari kuendelea kusaidia chuo hicho.
No comments:
Post a Comment