Wnaharakati
wa upinzani nchini Burundi wanaandamana kwa siku ya pili wakipinga
uamuzi wa kumtangaza Rais Pierre Nkurunziza kugombea nafasi ya urais kwa
muhula wa tatu.
Polisi walivunja maandamano kwa kutumia gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.Watu wapatao watatu waliuawa katika ghasi hizo nchini Burundi Jumapili wakati polisi walipofyatua risasi za moto hewani kuwatawanya waandamanaji.
Maelfu ya watu wamepuuza amri ya kuwataka kutokwenda kuandaamana mitaani katika mji mkuu Bujumbura.
Mwandishi wa BBC Maud Jullien anaripoti kutoka katika mitaa ya Bujumbura kwamba watu walioshuhudia matukio hayo wamemwaambia kuwa mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu Pierre Claver Mbonimpa amekamatwa katika jengo la chama cha waandishi wa habari nchini humo.
Awali alikitaka chama tawala kutomteua rais kuwania awamu ya tatu ya uongozi, akisema kufanya hivyo ni kukiuka katiba na mkataba wa amani wa Arusha.
Bwana Nkurunziza ametumikia nafasi ya urais kwa vipindi viwili, akiingia madarakani baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katiba ya Burundi inamruhusu rais kuchaguliwa mara mbili. Lakini wafuasi wa Bwana Nkurunziza wanasema anastahili kugombea kipindi kingine kwa kuwa alichaguliwa na bunge mwaka 2005.
Upinzani unasema hatua hiyo inatishia mpango wa amani ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005 vilivyodumu kwa miaka 12.
Zaidi ya watu 300,000 waliuawa katika vita hivi.
Waandamanaji wenye hasira Jumapili walirusha mawe na kuchoma matairi. Polisi walijibu kwa kufyatua mabomu ya gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha na kutumia risasi za moto, wakizuia maandamano kuingia katikati ya mji mkuu Bujumbura.
Waandamanaji wengi wamekamatwa.
Polisi pia wanatishia kukifunga kituo cha redio binafsi kama hakitaacha kutangaza moja kwa moja kuhusu maandamano hayo.
Rais Nkurunziza amesema katika uteuzi wake uliofanywa na mkutano maalum wa chama tawala:
"Ningependa kumwonya kila mtu: Kwa yeyote anayetaka kusababisha matatizo na chama tawala kilichochaguliwa na watu, atajikuta kwenye matatizo,"
Imeripoti Reuters.

No comments:
Post a Comment