Pages

April 25, 2015

Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka Mabalozi Wateule wa Urusi na Algeria

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Fedorovich Popov.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb). akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Urusi mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri aliishukuru Serikali ya Urusi kwa misaada inayotoa kwa Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile elimu. Wawili hao pia waliafikiana  umuhimu wa kukuza na kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.
Mazungumzo yanaendelea.
Waziri Membe akiagana na Balozi Mteule wa Urusi nchini Tanzania.
Waziri Membe katikati akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Urusi. Wakwanza kulia ni Balozi Joseph Sokoine, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kutoka kushoto ni maafisa wa Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania.
============================================
BALOZI MTEULE WA ALGERIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Algeria nchini Tanzania, Mhe.Saad Belabed.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Algeria nchini Tanzania. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Membe alieleza kuwa zaidi ya miaka 50 sasa Tanzania na Algeria zimekuwa katika uhusiano na ushirikiano mzuri wa nchi na nchi na hata katika ngazi ya Kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
Mazungumzo yakiendelea
Mazungumzo yanaendelea huku Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wa kwanza kushoto), Bi. Zuhura Bundala na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga wakinukuu mazungumzo hayo.
Waziri Membe akiagana na Balozi Mteule wa Algeria nchini Tanzania baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho.Picha na Reginald Philip.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...