Na Mwandishi Wetu
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe Mh.Subira Mgalu amezindua Shindano la Mama Shujaa
wa Chakula linaloendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam
kupitia kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika
kilimo na kumkwamua kiuchumi.
Subira
ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kumwezesha mwanamke
katika kilimo na kumkwa mwanamke kiuchumi iliyofanyika katika kijiji
cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Subira
amesema kufanyika kwa mashindano wilayani kwake ni fursa kwa wanawake
kushiriki kuchukua fomu za ushiriki na kuacha uvivu na kutaka zawadi
ya mshindi wa kwanza itokee wilyani humo.
Aliongeza
kuwa shindano hilo linawapa mwanamke uwezo wa kutambua haki zao umiliki
wa ardhi na kuwa na ubunifu wa kuweza kubadilisha mbinu za kisasa za
kilimo bora.
Nae
Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona amesema kijiji cha Kisanga ndicho
kitakuwa wenyeji wa shindano hivyo wanawake wa kisarawe wanahitaji
kujituma katika kuchangamkia fursa hiyo.
Pia
Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa
Kisarawe kuwaruhusu wake zao na watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa
wingi na kushiriki katika shindano hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya fursa
ambazo watazipata kupitia Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo wakati uzinduzi
wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 akizindua Rasmi Mashindano
hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.
Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam,Eluka Kibona akielezea Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
Diwani
wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akizungumza na Wakazi wa
Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
Kikundi cha sanaa cha Sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
Mwenyekiti
wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica Sijaona
akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na kuchukua fomu
ili waweze kuungana na akina mama wengine pindi Shindano la Mama Shujaa
wa Chakula litakapoanza.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Kisanga Bwana Mohamed Mlembe Akiwashukuru Oxfam kwa
kuleta Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 Kijijini kwake.
Mh.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akifurahi kwa Burudani ya
Muziki pamoja na wananchi baada ya uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama
Shujaa wa Chakula kijijini Kisanga.
Mwakilishi
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo Akiongea na
wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia kuona
umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi na Haki
zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua Mama
kiuchumi.
Mh.
Subira Mgalu akifurahi pamoja na Baadhi ya kinamama wa kijiji cha
kisanga Baada ya Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.
Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu za kushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015.
Baadhi ya Wageni waalikwa na wananchi wa Kisarawe wakiwa katika Sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Wilaya
hiyo wakto akizindua shindano la Mama Shujaa lililofanyika leo katika
Kijiji cha Kisanga wilayani humo.
No comments:
Post a Comment