Keki
maalum iliyoandaliwa kwenye sherehe za uzinduzi wa shamra shamra za
miaka 70 ya Umoja wa Mataifa uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hoteli
ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati)
akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN
Women nchini Tanzania, Anna Collins kabla ya zoezi la kuwasha mishuma 70
kwenye cake hiyo ikiwa ni uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya
Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Mshehereshaji wa sherehe hizo Afisa Habari
wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili
kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women
nchini Tanzania, Anna Collins wakiwa wamejumuika na wafanyakazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye mnuso huo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili
kushoto) akiwasha nakshi nakshi zilizowekwa kwenye cake maalum ya
uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
Anayemkingia upepo ni walioandaa Cake hiyo kutoka kampuni ya M.E Gift
Wraps and Delivery huku Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins naye akijianda kufanya zoezi
hilo.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakishiriki kuwasha mishumaa 70 iliyowekwa kwenye cake hiyo.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakikata cake kwa niaba ya wafanyakazi wenzao.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia)
akila kipande cha cake kwenye mnuso huo.
Wafanyakazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakilishana cake kabla
ya kupata chakula cha usiku wakati wa shamra shamra za uzinduzi wa
miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi wenzake.
Pichani
juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
wakijumuika kwenye chakula cha usiku wakati wa sherehe za uzinduzi wa
shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifuatiwa
na Afisa Habari wa UNIC, Usia Nkhoma Ledama wakipakua chakula cha jioni
kwenye mnuso huo.
Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakijisevia nyama choma ndani ya hoteli ya White Sands.
No comments:
Post a Comment