Siku
mbili tu zimesalia kabla ya pambano la kimataifa la ngumi kati ya mastaa
wawiliManny Pacquiao na Floyd Mayweather ambao watapanda ulingoni na
kutegua kitendawili cha nani mkali zaidi.
Hili
pambano ni kama dunia nzima inalisubiri kwa hamu yani.. vyombo vya
habari vimelipa promo kubwa kiasi cha kwamba hata ambao hawafuatilii
ndondi imebidi wafuatilie hawa jamaa ni akina nani hasa !!
Jana
nilikusogezea pichaz zikionesha Manny Pacquiao akiingia zake Las Vegas
na msafara kabisa wa pikipiki, basi kubwa na gari nyingine
zikimsindikiza.
Leo ni zamu ya Floyd Mayweather ambaye ametumia muda wake kwenda kukagua ukumbi wa MGM Grand ambao utatumika kwa pambano lao.
Ukumbi ulifurika mashabiki.. camera za mapaparazzi nazo hata hazikuwa mbali.
Pambano
hilo linatajwa kuwa pambano la kifahari zaidi duniani na ambalo
viingilio vyake ni vikubwa ukilinganisha na mapambano mengine yaliyowahi
kufanyika duniani.
No comments:
Post a Comment