|
Kijji cha Amani kinavyoonekana |
Taasisi
ya Better Living Aid kupitia kampuni ya Royal Nsyepa General
Supplies ambayo mkurugenzi wake ni Bw Mgalula Fundikira za jijini Dar es
Salaam leo imepeleka mtaalamu wa upulizaji madawa ya kuuwa wadudu kama
kunguni na wengineo katika kijiji cha Amani kilichopo km 6 nje ya mji wa
Tabora.
Hatua
hiyo ya Better Living Aid ilifuatia ombi toka kwa wakazi wa kijiji hicho
chenye wakazi wapatao 70 ambao baadhi yao ni wazee na wenye uathirika
wa gonjwa sugu la ukoma, pamoja na changamoto ya kunguni pia wakazi wa
hao wametoa maombi kwa taasisi hiyo nawasamaria wema wengine wajengewe
vyoo zaidi kwani kwa sasa wana vyoo viwili tu vilivyo kwenye hali ya
kutumika, huku vingine vikiwa vimejaa na haviwezi kunyonyeka.
Akiongea
na mtandao huu mwenyekiti wa kijiji hicho Bw George Lusambilo
alisema"kwa kweli tunaishukuru sana taasisi hii kwa kutuletea msaada
huu, kwani tumekuwa tukilala kwa taabu sana, naona kuanzia leo tutalala
kwa raha kama watu wengine" pia aliongeza "Ila tu jamani msituchoke,
bado tunakumbushia ombi la kujengewa vyoo zaidi kwani idadi yetu na
ukilinganisha na vyoo tulivyonavyo kwa kweli ni changamoto, lakini pia
tunaomba tupate hata ka zahanati kadogo ili mganga na muuguzi wapate
mahala maalum pa kutuhudumia hasa sisi wagonjwa wa ukoma"
Naye
afisa ustawi wa jamii mkoa Bw Charles Makoye alisema "kwa niaba ya
serikali naishukuru sana tasisi hii ya Better Living Aid kwa jitihada
zao za kuboresha maisha ya wakazi wa hapa kijijni na napenda kuchukua
nafasi hii kutoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kusaidia kijiji
hiki kwani ustawi wa jamii si suala la serikali peke yake bali ni la
jamii nzima inayotuzunguka kwani hawa wazee wametoka huko huko katika
jamii zetu.
Mratibu
wa taasisi ya Better Living Aid ametoa wito kwa makampuni na watu
binafsi kuiunga mkono taasisi hiyo katika jitihada zake za kuwajengea
vyoo na zahanati wakazi wa kijiji hicho. Vile vile ameeleza dhamira ya
taasisi hiyo kutafuta wafadhili ili kujenga zahanati katika kijiji cha
Masweya, wilayani Ikungi mkoa wa Singida alisema "Nilipata kufika
kijijini Masweya mapema mwaka huu ambako nilipata kujua kwamba wakazi wa
hapo hulazimika kutembea km 30 na ushee kwenda kjiji cha Mtunduru
kupata huduma za matibabu. Hivyo Better Living Aid itafanya kila
liwezekanalo kijiji hicho kipate zahanati japo mdogo ya kuweza kuhudumia
wagonjwa wa Malaria nk pia zahanati iweze kutoa huduma kwa wazazi, kitu
mambacho kwa sasa hakipo kjijini Masweya.
Shukurani
za dhati ziwaendee Mh Munde Tambwe (viti maalum Tabora), Mh Aden Rageh
(Mbunge Tabora mjini) Bibi Joha Masawe, Bi Mtagwa Fundikira, Bibi Jamila
Kaimika, Bibi Celina Koka na wanachama wote wa kundi la Better Living
Aid Tunashukuru kwa msaada wa hali na mali iliyowezesha kijiji cha Amani
kufanyiwa fumigation bila kumsahau mtaalamu Bw Selemani Muhogo wa
kampuni ya SILVER ENTERTRADE LIMITED aliyepulizia dawa hiyo.
|
Baadhi ya magodoro ya wakazi hao yakiwa yametayarishwa kwa kupuliziwa dawa |
|
Bw Muhogo akiandaa mashine ya kupulizia dawa |
|
Hapa akianza kunyunyiza dawa kwenye magodoro |
|
Job DONE |
|
Baadhi ya vyoo vya hapo kijijini |
|
Mzee Hamisi Husseni akisubiri vifaa vyake vitiwe dawa |
|
Badhi ya mizigo ya wakazi wa kijiji hicho |
|
Afisa ustawi wa jamii Bw Charles Makoye akiongea na mkazi wa kijini hapo. |
Bibi Theresia Joseph akiwa nje ya chumba chake akisubiri huduma ya kupuliziwa dawa ya kuuwa kunguni na wadudu wengine. |
|
|
Mahindi yakiwa yamewekwa nje kwa muda kupisha upulizaji dawa ya kuua kunguni ndani ya chumba yalimokuwa yamehifadhiwa. |
|
Blogger wa Aloyson.com akiwa na Mzee Hamisi Husseni |
|
Mratibu
wa taasisi ya Better Living Aid, Mkala Fundikira kushoto akiwa na
mwenyekiti wa kijiji cha Amani Bw George Lusambilo baada ya zoezi la
upulizaji dawa ya kuuwa wadudu kunguni waliokuwa wakwasumbua mno wakazi
wa kijiji hicho cha wazee wasiojiweza na waathieika wa ugonjwa wa ukoma. |
|
Baada ya ya kupuliziwa dawa baadhi ya kunguni wanaonekana wakiwa wamekufa. |
|
Blogger Juma Kapipi wa JHabari blog akiongea na mhanga wa kunguni baada ya kumhoji |
|
Baadhi ya nguo zikichomwa moto baada ya kukutwa na kunguni wengi kupita kiasi. |
Habari na picha kwa hisani ya TBN Central zone!
No comments:
Post a Comment