Katibu Mkuu Wizara ya
fedha Bw. Servacius Likwalile (kushoto) akisaini Mkataba wa mkopo wenye
masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya
kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo
Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es
salaam. Kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero
akisaini mkataba huo kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald
Kaberuka.
Katibu Mkuu Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando (kushoto) akitoa neno la
shukurani baada ya kusainiwa Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu
kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo
cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza
kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero na katikati
ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile.
Katibu
Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile (kushoto) akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam wakati wa
kusaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo
ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya
moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS).
(Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO).
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
12/12/2014.
Serikali
ya Tanzania imetiliana saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu
wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 9.4 ambazo ni sawa na Sh.
Bilioni 15.5 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya
kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo
Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Mkataba
huo wa makubaliano umesainiwa leo jijini Dara es salaam na Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya
Tanzania na Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero kwa niaba
ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka.
Dkt.
Likwelile alisema kuwa kituo hicho kitasaidia kupunguza tatizo la
wataalam wa afya nchini na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na
hivyo kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi.
Kwa
upande wake Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero
ameipongeza Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusaini mkataba huo kati ya
nchi nne za jumuiya ya EAC zinazokusudiwa kujenga kituo kama hicho.
Bi
Tonia alisema kuwa benki ya ADB imejiwekea lengo kuboresha rasilimali
watu katika fani ya afya ambapo mradi wa ujenzi wa kituo kinachojengwa
MUHAS upo katika mkakati wa benki hiyo ambao uulianza 2011 hadi 2015,
mpango mkakati wa benki wa 2013 hadi 2017 na mfumo mpya wa elimu katka
nchi za Afrika.
Mfumo
huo unalenga kutatua tatizo la utaalaam katika soko la ajira kwa
kupitia vituo bora vya kanda vya afya ili kuendana na dira ya maendeleo
ya Taifa na mkakati wa kupunguza umasikini ifikapo mwaka 2025.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan
Mbando ameushukuru uongozi wa benki ya ADB kwa kuendelea kushirikiana na
Tanzania na kuahidi fedha hizo zitatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Hadi
kukamilika kwa kituo hicho cha afya kinachojengwa katika chuo cha MUHAS
kitagharimiwa na benki ya ADB kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment