Miss World 2014, Rolene Strauss aliyeiwakilisha South Africa akifurahi baada ya kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014.
Leo December 14 kwenye Historia ya mwaka 2014, Mashindano makubwa ya
Miss World 2014 yalikuwa yakifanyika London, Uingereza ambapo washiriki
mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa Tanzania, Happiness
Watimanywaakiwa mmoja ya washiriki hao.
Mpaka leo asubuhi matokeo ya kura ambazo zilikuwa zikipigwa na watu
zilimuweka mwakilishi huyo kuwa katika nafasi ya pili, akitanguliwa na
Miss Thailand ambapo iwapo Happiness angekuwa namba moja basi ilikuwa
moja kwa moja aingie kwenye Top 10 ya mashindano hayo.
Kutokana na Hapiness kupitwa kura na Miss Thailand hakufanikiwa
kuingia kwenye Top 10, huku katika wale waliotajwa ni wawakilishi wawili
pekee, mmoja wa South Africa na mwakilishi wa Kenya waliofanikiwa
kuingia Top 10.
Mwakilishi wa South Africa, Rolene Strauss amefanikiwa kuvuka hatua zote na hatimaye kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014, nafasi ya pili ikishikwa na Miss Hungary, Edina Kulcsar na nafasi ya tatu kushikwa na Miss USA, Elizabeth Safrit
No comments:
Post a Comment