Baada ya Miss South Africa
anajulikana kwa jina la Rolene Strauss ambaye ndie mshindi wa taji la
Miss World 2014, Aliyekuwa akiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo
kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram amefunguka baada ya kushindwa
kunyakua taji hilo na hichi ndicho alichokiandika
Nampongeza @rolenestrauss (South
Africa) kwa kuibuka mshindi Miss World 2014.Watanzania wenzangu na
marafiki kutoka mataifa mengine, tumepiga kura sana, mmeonyesha support
kubwa kuliko matarajio ya wengi bahati mbaya kura hazikutosha.
Natumia nafasi hii kuwashukuru wote
mmoja mmoja kwa kuniunga mkono kwa kipindi chote ambacho nilikua hapa
jijini #London na tokea niliposhinda mashindano ya #MissTanzania.
Nisingefika hapa bila support yako. From deep inside my heart. I thank
you.
Kuanzia aliyetumia muda na pesa
yake kunipigia kura, aliyeandika na kutangaza habari yangu, designers
mbalimbali, familia yangu, marafiki wote, wote, wote, I thank you.
Nimejifunza vitu vingi sana kipindi
chote hiki na kwakweli watanzania tumeonyesha umoja wa hali ya juu
sana. Umoja wetu na udumu katika mambo yote ya kimaendeleo kwa taifa
letu.
Mbarikiwe
#Happiness4MissWorld
Rolene Strauss mwenye umri wa miaka 22
akiwa ni mwanafunzi wa chuo cha udaktari katika chuo kikuu cha Free
State (University of Free State) Rolene alifuatiwa na mshindi wa pili
amabye jina lake ni Miss Hungary Edina Kulcsar.
No comments:
Post a Comment