Pages

December 12, 2014

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA KATA ZA MIKUMBI,NDARO NA MBANJA HUKO LINDI MJINI KWA AJILI YA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.



Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Regina Chonjo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi tarehe 11.12.2014.




Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi wa CCM Kata ya Mikumbi iliyoko Mjini Lindi wakati alipowasili kwenye eneo hilo kwa ajili ya kufanya mkutano wa ndani na viongozi hao tarehe 11.12.2014. Anayemtambulisha kwa wajumbe hao ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Mikumbi Bwana Bakari Seif Mikojo.

Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa chama wa Kata ya Mikumbi katika mkutano wa ndani wa Chama hicho kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini tarehe 14.12.2014.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na uongozi wa Chama wa Kata ya Ndoro iliyoko Lindi Mjini mara baada ya kuwasili katani hapo kwa lengo za kuzungumza na viongozi wa kata hiyo kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014. Anayetambulisha ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo Ndugu Saleh Ahmed Saleh.



 Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishirikiana na viongozi wa CCM wa Kata ya Ndaro kuunga mkono muundo wa serikali mbili unaopendekezwa na Rasimu ya Katiba.

Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na uongozi wa Kata ya Ndaro katika mkutano wa ndani kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini tarehe 14.12.2014.

  
Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwatambulisha na kuwaombea kura wagombea uenyekiti wa serikali za mitaa wa Kata ya Ndaro kwa wajumbe wa mkutano. Mama Salma yuko Wilayani Lindi Mjini kuhamasisha wananchi kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014.

Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mbanja kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika tawi la Mto Mkavu katika wilaya ya Lindi Mjini tarehe 11.12.2014.
PICHA NA JOHN  LUKUWI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...